google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mke wa Mtu Amua kuvua Nguo Baada ya Pombe Kumpanda Kichwani | UDAKU SPECIAL

Mke wa Mtu Amua kuvua Nguo Baada ya Pombe Kumpanda Kichwani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KITUKO cha aina yake kimejiri Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa ikitumbuiza

Katika onesho hilo, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu alifanya kitendo cha aibu baada ya kusaula nguo zake zote na kubakia na nguo za ndani.

Katika onesho hilo, Extra Bongo ilikuwa ikiwashindanisha mashabiki wake kucheza staili yao ya Kizigo na washindi kujinyakulia zawadi za fedha.

Wakati bendi hiyo inayoongozwa na ‘Kamarade’ Ally Choki ikitoa burudani, ghafla mwanamke huyo  alivamia jukwaa na kuanza kucheza kwa staili aliyokuwa akiijua mwenyewe.
Picha zaidi Click Read More



Mpigapicha wa amani  alipojaribu kumpiga picha dada huyo alihamaki na kumjia juu huku kumtishia kumvunjia kamera yake huku akidai kuwa yeye ni mke wa mtu, hivyo hapaswi kupigwa picha.

“Mimi ni mke wa mtu ukifanya mchezo nitakutolea laana,” alisema mwanamke huyo huku akizishika nguo zake na kuanza kuzitoa mwilini mwake  moja baada ya nyingine.

Wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi lake la kusaula nguo, alijitokeza dada mwingine ambaye  aliambatana naye pamoja ukumbini hapo na kumwita  kwa jina la wifi.

“Wifiii…, wifiii…, weee wifii pombe gani hizo, usivue nguo, usifanye hivyo ni aibu,  itakuwaje kaka akiziona hizo picha magazetini?” alisema dada huyo aliyedaiwa kuwa ni wifi mtu lakini pamoja na kumpigia kelele hizo haikusaidia kumzuia  mwanamke huyo mcharuko kusaula nguo zake.

Baada ya kuombwa sana na wifi yake, mwanamke huyo alivaa nguo zake na kuendelea na burudani hadi mwisho.

Haikufahamika mara moja kama mwanamke huyo alifanya  kitendo hicho kutokana na pombe au hasira za kupigwa picha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad