CCM, Chadema Dar wamgeuzia kibao JK

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni nadra kutokea lakini wafuasi wa vyama vya siasa vya CCM na Chadema, wameungana kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu kero ya maji eneo la Kimara-Golani, Dar es Salaam.

Rais Kikwete alikutana na hali hiyo wakati akifungua Daraja la Kimara jana, tukio hilo liliwakusanya watu wengi hasa wanachama wa CCM na Chadema waliokuwa wamevalia sare za vyama vyao.


Wafuasi wa Chadema waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa Chadema, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.


Akizungumza baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Kikwete aliahidi kuitisha kikao Jumatatu ijayo kitakachomhusisha Profesa Maghembe na maofisa wa wizara yake, wabunge wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, wakuu wa wilaya ili kuweka mikatati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.


“Ninaomba Machi 25... tukutane ili tuweke mikakati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hili,” alisema Rais Kikwete.


Akiwa Hospitali ya Mwananyamala, Rais Kikwete alizindua maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi na akazungumzia suala la dawa za kulevya kwa kusema atahakikisha mapambano yanaendelea kwani dawa hizo zinaua nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad