H Baba Ajifagilia kuwa Ndio Msanii Aliye Piga Show Nyingi Mwaka Jana-Mashabiki Wagoma

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakiamini msanii aliyepiga show nyingi zaidi mwaka jana ni Diamond.
 

Kwa mujibu wa H.Baba, yeye ndiye msanii wa Bongo Flava aliyepiga show nyingi zaidi mwaka jana. Ameiambia 255 ya Clouds FM kuwa mwaka 2012 amepiga jumla ya show 625!


Msanii huyo ambaye mwaka jana aliingia kwenye mgogoro wa wimbo “Nataka Kulewa” na Diamond amesema show hizo ni pamoja na zile za promotion Za makampuni mbalimbali na zake binafsi. Anasema miongoni mwa show hizo ni zile alizokuwa akilipwa zaidi ya shilingi milioni 2.
 
Hata hivyo watu wengi wameonesha kuwa na wasiwasi na idadi hiyo ya show hasa baada ya kudai kuwa show hizo amekuwa akizifanya siku za weekend. Haya ni maoni ya baadhi yao kama walivyoandika kwenye ukurasa wa Facebook wa Dj Fetty.
 
Elizabeth Benedict
hahhaha,,nmemckia anaongea tena anahema kama katoka zoez la ngumi,duuuuh kama uongo unaenda kwa elimu bas H-BABA yey n PhD holder,,kwa navoifaham calculator ijumaa,jmos na jpil kwa mwez zpo 12 sasa kwa miez 12 ztakua 144 hapo nshamuongezea na za mwez wa pil japo znakuaga 9 ila nmemfanyia 12 yan kwa kumsaidia tuuu na kumkamata vzuri,,ama anafanyaga kwa ijumaa show 4,jmos show5 na jpil show 5 hapo sawa ila hv hv HAPANA au may b amejumlisha na zle ambazo anafanyaga akiwa na FURURAhh…hahahah,,,its shav.
 
Eras Rweyemamu
Me mziki wa bongo siujui fresh ila h baba ye huwa anafanya show mikoani na kongo huko hapa dar huwa hana soko inawezekana tu hata afanye chumbani kwa mtu ni show ye anahesabu nyie si mlitaka diamond aseme ivo ili mrembeshe story? Dj fetty b’ana
 
Michael Minja
Kwa mahesabu hayo sio kweli maana kama anafanya shoo kwa week mara tatu yani ijumaa juma mosi na juma pili basi kwa mwezi anatakiwa afanye show 18 ambapo ukizidisha kwa miezi 12 unapata show 216 tena hapo awe hajamiss show hata moja hivyo kwa mahesabu alioyatoa yeye ya show 625 nina hakika atakuwa amekosea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad