Mastaa wa Kike Bongo Wazalishwa na Kulea Watoto Wenyewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katika ulimwengu wa mastaa wa kibongo kuna vijimambo kibao mojawapo ni wale wa kike kujiingiza kwenye kamchezo ka mapenzi na kudanganywa kilaini kisha kushiriki mchezo wa kikubwa bila usalama.

Matokea yake ni kuzalishwa na kuachwa solemba huku wakilea watoto wao wenyewe..
Gazeti la Ijumaa Limetoa list wa Mastaa Kumi ambao wana watoto lakini hawajaolewa huku wakielea watoto wao wenyewe..

1.Shilole
Huyu ni Star wa Filamu pamoja na Music...Huyu mpaka sasa ana watoto wawili kwa wanaume tofauti ...kwa sasa anaishi na kuwalea watoto wake yeye mwenyewe na juzi kati aliongea katika redio moja na kusema yupo Single kwa sasa.

2.Isabela Mpanda
Huyu ni model na alishawahi kushinda taji la miss Ruvuma 2006 , yeye ana watoto wawili pia kwa kutoka kwa wanaume tofauti ...Anamshukuru mungu kuwa ana uwezo wa kuwalea watoto wake mwenyewe.

3.Jini Kabula (Mariam Jolwa)
Alianza kwenye maigizo ya runinga kisha akaingia kwenye umiss kidogo na sasa muziki , yeye alizaa na Mr Chuzi ila mapenzi hayakudumu ...Japo Nasikia MR Chuzi anampa tafu katika kulea Mtoto.

4.Jack Chuzi
Huyu alianza kwenye urembo na kisha kuingia katika maigizo ..ana mtoto mmoja ambae anamlea mwenyewe..Alizaa na mwanaume ambae hakumtaja jina.

5.Nora
Huyu ni mwigizaji wa siku nyingi aliolewa na kupata mtoto mmoja ila ndoa haikudumu na sasa analea mtoto mwenyewe

6.Jack Maisha Pluz
Alipa Umaarufu Akiwa Maisha Plus kabla ya kujiingiza kwenye filamu ..Aliachwa Solemba baada ya kuzalishwa na mvulana hadi sasa hana mawasiliano nae

7.Snura Mushi
Alianza kwenye maigizo na sasa kwenye filamu ana mtoto mmoja wa kike anasema toka akiwa na mimba hana mawasiliano na baba wa mtoto wake

8.Sister Fay
Huyu hasikiki sana ila nae yumo ni mwigizaji na pia mwanamuziki ana mtoto mmoja aliyejifungua mwaka jana anakiri kuachwa njia panda na mwanaume aliye mzalisha

9.Maunda Zoro
Huyu ni mdogo wa baba Zoro Ana mtoto mmoja , na huwa hapendi kumsema baba wa mtoto wake ila mpka sasa anaishi nyumbani kwao kwa baba na mama

10.Monalisa
Huyu ni mwigizaji mkubwa , aliwahi kuolewa na muongoza filamu George Tyson na kuzaa nae na kisha kuachana nae na akaolewa tena na mtu mwingine na kuzalishwa tena ila sasa nae yupo peke ake na kuwalea watoto wake mwenyewe.




-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tabia zao chafu ndio zinawafanya wasiolewe wao ni wa kuzlishwa tu hawafai kuwa mama wa famlia

    ReplyDelete
  2. Mbona mastaa wa kike pekee.!!!?

    ReplyDelete

Top Post Ad