Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ajinyonga Mpaka Kufa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo cha Sheria, Joseph Bernadina (25), amejinyonga kwa kutumia kamba na kukutwa ameifunga juu ya mti, katika eneo la Yombo chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha  kutokea kwa tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.

Aliongeza kuwa Jumamosi iliyopita alipokea simu kutoka kituo cha polisi cha chuo hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi alitishia kujiua, lakini aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka kitengo maalum cha washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa Jumapili.

“Nilikuja tena kushituka leo asubuhi napokea simu kutoka kwa mshauri wa wanafunzi kuwa kuna wanausalama wamemkuta mwanafunzi akiwa amejinyonga juu ya mti huku akiwa na karatasi kwenye mfuko wa sharti ikimtambulisha pamoja na ujumbe uliosema, kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote kwani amejiua kwa ridhaa yake --asisumbuliwe mtu yeyote kwani nimefanya hivi kwa maamuzi yangu mwenyewe pia nizikwe kwetu--” alisema.

Profesa Mgaya alisema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na Uongozi wa chuo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu na kwamba Chuo kitagharamia kuusafirisha mwili kama alivyoomba katika ujumbe aliouacha wa kupelekwa wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa.

Naye rafiki wa marehemu, Daniel Mwamlima, alisema marehemu hakuwahi kuzungumza chochote kilichoashiria kuwa ana matatizo wala mgogoro na mtu yeyote.  Alisema walimuacha hospitalini Jumamosi na kesho yake kumchukua, lakini  baadaye aliwatoroka.

“Sasa leo (jana) asubuhi tulipata taarifa za mwanafunzi kujinyonga mbaya zaidi tukakuta ni yeye,” alisema Mwamlima.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Yasini Athumani, alisema wamezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio na alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba marehemu aliwahi kuwa na historia ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu ya ugonjwa wa msongo wa mawazo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hana ki vzuri huyo

    ReplyDelete
  2. ukiwa namawazo nibora ushirikishe watu,mm nlishawahi kujaribu kujiua kwa klorokwin 20,km maika 14 iliyopita.ilikua usiku nikajifungia chumbani nikiwa na mtoto wangu mdogo,lol nilihis joto kali sn! sikujua kilichoendelea nilishtuka saa 2 asbuhi nikamkuta mwanangu ananiangalia tu!! niliogopa saaaana! nilipiga magoti nikamuomba M'Mungu msamaha,namwanangu pia.hua naumia sn nikikumbuka hiki kitu.

    ReplyDelete
  3. sijui alikuwa na mkopo maskini! Maana misongo hii wakati mwingine inasababishwa na ukata na ugumu wa maisha vyuoni, serikari hainabudi kulishughulikia hili kwa kina.

    ReplyDelete
  4. poleni sana wazaz wake jaman!......hiv kwa nn jaman inaumiza sana!

    ReplyDelete
  5. R.i.p master jus coz of stress...!

    ReplyDelete
  6. Mbona habari inasema amejinyonga kwenye mti... na hii picha inaonyesha ni ndani?
    Confusing!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad