Simba:Sakata la Rage Kuenguliwa Madarakani Kuamuliwa Kisheria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Hatima ya kubaki madarakani kwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage itaamuliwa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoongozwa na wakili Alex Mgongolwa.

Hatua hiyo imefikiwa na TFF baada ya kupokea barua kutoka kwa uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wa Simba na kufanyika juzi kwenye Uukumbi wa Starlight, Dar es Salaam na kumwengua madarakani Mwenyekiti wa Simba, Rage.

Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake na mMkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu yao.

“Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili, Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo na kutoa hatima ya Rage,”alisema Wambura.

Hata hivyo Wambura alisema TFF inawasisitizia wanachama wake ikiwamo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad