google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Anataka Awe Nyumba Ndogo Yangu:Nifanyeje? | UDAKU SPECIAL

Anataka Awe Nyumba Ndogo Yangu:Nifanyeje?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wapendwa habari za majukumu ya kulijenga taifa.
 Nikiwa katika pitapita zangu miezi mitatu iliyopita; nikikutana na mwanadada mrembo; nikawa nimekaa naye meza moja. Katika kuongea ongea akanipa historia ya maisha yake. Kikubwa ni kwamba aliolewa lakini tabia ya mume wake kumpa kichapo mara kwa mara aliamua kuomba uamisho kazini na kuhama toka kwenye mji anapoishi mume wake.
Kwa kuwa tuliendelea kuwa na mawasiliano; siku moja akanikaribisha nyumbani kwake; nikakuta amejiandaa kisawasawa; mambo ya kikubwa yakaendelea, jioni nikatoka naye out; haikuishia hapo tukaendelea kama wapenzi. Majuzi ananambia eti anataka anizalie mtoto na anitambulishe hadi kwa ndugu zake.
Nashindwa kumpa ok kwa kuwa mi tayari nina mke; na mume wake bado anambembeleza warudiane. Yeye anadai awezi kurudiana na huyo mwanaume kwa sababu ni mkorofi na anamdunda mara kwa mara; mtoto wa watu ana makovu hadi namuonea huruma. Naomba ushauri wako we unayesoma hii habari.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuhsu kuzaa naye mmmmh hapana ila kuendelea kumpa kitu haina noma endelea naye tu hakuna tatizo mkuu.

    ReplyDelete
  2. sasa unataka ushauri gani wkt ana akili yako,hujasema kama umeoa ila kama una mke pepo la ngono litakuwa linakusumbua,make nadhani ungemwambia kuwa huwezi kumsaliti mkeo

    ReplyDelete
  3. Endelea kula kisamvu ila jamaa akikubamba utajuta kazaliwa, kama vip tema na naye kabisa kama unayathamin maisha yako coz jamaa ataona wew ndio unampa kiburi.

    ReplyDelete
  4. Usiwe Diamond mwingine

    ReplyDelete
  5. wewe unaiba threads za watu wa jf huwiiiiii yaani huwezi anzisha yako????

    duh huwezi tafuta story zako mwenyewe au watu wakurushie?

    ReplyDelete
  6. yaani unaiba mambo ya mapenzi jamii forum duh aibu.

    nimekuta zote nishazisoma na wanaorusha jamii forum ni watu tofauti ndio maana nimejua unaiba maana auweki source

    ReplyDelete
  7. Utakojoa dagaa

    ReplyDelete
  8. KWAN WEWE HUNA NKE ULIANZAJE KUMKUBALIA HUYO DADA?

    ReplyDelete
  9. ww kzbo mkubw angalia angalia mtabadlishan nay atachkua mkeo ucnune shanglia

    ReplyDelete

Top Post Ad