Bayern yaisambaratisha Barca

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Munich, Ujerumani

Bayern Munich imejisafishia njia ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuichapa Barcelona kwa mabao 4-0  katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza, wakati leo Borussia  Dortmund wataonyesha kazi na Real Madrid.

Bayern wakiwa kwenye uwanja wao wa Allianz Arena walipata mabao yao kupitia Thomas Muller aliyefunga mabao mawili huku Mario Gomez  na Arjen Robben wakifunga bao kila mmoja.

Muller alifungua karamu hiyo ya mabao katika dakika 25 akifunga goli lake kwa kuunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na Dante.

Mabingwa hao wa Ujerumani waliendeleza kasi na kufanikiwa kupata  bao la pili lililofunga na Gomez akiunganisha kichwa kilichopigwa na Muller katika dakika 47,  kabla ya  Robben kupachika bao la tatu kwa shuti la chini  lililomshinda kipa Victor Valdes katika dakika 73, wakati

Barca wakiwa hawaamini kinachotokea Muller alipachika  bao la nne kwa kuunganisha vizuri krosi ya John Alaba.

Leo mabingwa wa kihistoria Real Madrid watakuwa na  kibarua kigumu mbele ya Dortmund katika mchezo mwingine  unazikutanisha timu za Hispania dhidi ya Ujerumani. Dortmund inajivunia rekodi yake ya kuifunga Real katika hatua ya makundi msimu
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad