Maneno Aliyoyasema Mke wa Godbless Lema Baada ya Kukamatwa na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Taarifa za sasa kutoka Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.

Taarifa za uhakika kutoka kwa mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.

Namkariri Mke wa Lema akiongea na TheTZA millardayo.com akisema “jana usiku saa sita kasoro watu walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka kuitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia gari mbona chochote hakikutokea?”

.

“Baada ya muda kusogea ikabidi Lema aanze kuwapigia marafiki, jamaa na baadhi ya viongozi wa Chadema, kabla ya hapo pia tuliamua kupiga kengele ya kampuni ya security ambao muda mfupi baadae walikuja na gari yao huku Polisi wakiendelea na vitisho kwamba watapiga mabomu na kuvunja ukuta la sivyo Lema ajisalimishe, Viongozi wa Chadema na marafiki walipowasili wakamshauri Lema ndio akajitokeza wakati huo ni saa tisa usiku” – Mama Lema

“Alipojitokeza Polisi walimchukua na mimi nikaondoka nao, tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa maelezo lakini alikataa na kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa rumande, asubuhi tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye kikao na haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi ikamalizika jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka Jumatatu” – Mama Lema

“shitaka kubwa lililo mbele yake ni uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo cha Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye maelezo Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga” – Mama Lema

Kwa kumalizia, Mke wa Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale waliolivuta, gari liko zima kabisa………… toka nimeolewa na Lema nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake ya kwanza kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za Ubunge” (31)
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu atusaidie serikali yetu inatia aibu,kwa kukosa utawala wa sharia.je wanasheria wa Tanzania na wasomi,na rais wa nchi haya mambo anaona ni sahihi?,uongozi wa jeshi la wananchi hawaoni ,wanakila sababu ya kusimamia ulinzi wa raia na mali zao ?kama polisi wameshidwa?,kunahaja ya kufunja jeshi la polisi,nakuchagua vijana wa vyuo au wenyehekima kuwa wakuu wa mikoa,inakuwa kama vile tuna miaka 5 tangu uhuru ,Mungu tusaidie ,hata loliondo uliuzwa hivihivi,.

    ReplyDelete
  2. saikologia ya polisi wetu,na wasaidizi wa mkuu wa mkoa,hawawezi kusoma mazingira na behavior za watu,na kutoa maamuzi mazuri,km mkuu wa mkoa anaweza kuongea hivi ,inakuwaje?,uzalendo utawale Tanzania na sio vyama vya siasa,wafe wanafunzi wangapi?,ndipo serikali ishuhulikie matatizo ya wananchi,mwanasheria wa manispaa,huwa anafanya nini?wale polisi walikuwa na busara arusha walienda wapi?Taarifa za Tanzania sinasomwa sana nje ya nchi kuliko tunavyo fikiria,kuna watu wanafuatilia nchi hata miezi 6 kabla ya kutembelea nchi husika.vyombo vya usalama vishirikiane wasiende polisi tu kwenye matukio km haya jeshi la wananchi lihusishwe hasa ktk mikoa km wa arusha,wenge weza kumshauri mkuu wa mkoa ,kuliko kuaibisha Tanzania hivi,anafanana na yule waziri alidai Tanzania ni muungano wa visiwa wa Zanzibar na Zimbabwe,tumekosa nini? mbona tuna toa nafasi ya kudharauliwa hivi ktk ngazi ya kimataifa,TATUA TATIZO sio kumshika MBUNGE,FOR sure we need pray to solve our problem like this still we have graduate from college and university there don't have work ,why do we have some one in the wrong place at the wrong time.
    .

    ReplyDelete

Top Post Ad