Ndege mbili za FastJet Zaondolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndege mbili za kampuni ya
FastJet zimeondolewa kwenye
safari zake na kusababisha
usumbufu kwa wateja
wanaotumia usafiri huo.

Kampuni hiyo inakabiliwa na
hali tete baada ya kudaiwa
kuwa wasafiri wake kukosa
huduma ya vinywaji na chakula.

Kufutwa kwa safari kulitokea
kipindi kifupi baada ya uongozi
wa kampuni hiyo kuitisha
mkutano na waandishi wa
habari na kueleza kuwa wana
mpango wa kuongeza safari katika maeneo yenye vivutio
vya utalii.

Hivi karibuni, FastJet iliamua
kusimamisha huduma ya ndege
zake mbili kwa madai ya mvua
nyingi zinazoendelea kunyesha
nchini.

Kutokana na uamuzi huo,
kampuni hiyo imeandika barua
kwa mawakala wa kukatisha
tiketi kuwaelekeza kurudisha
fedha kwa abiria waliokuwa
wamewakati tiketi.

Katika taarifa yake kwa mmoja
wa wakala wa kukatisha tiketi
(jina tunalo) kampuni ya Fastjet
inasema kuwa inasikitisha
kumjulisha wakala huyo kuwa
imebadilisha muda wa safari za ndege yake.

"Tumesimamisha safari kama
ifuatavyo. Kilimanjaro kwenda
Mwanza kwa ndege namba FN
141/142. Kilimanjaro kwenda
Zanzibar kwa ndege namba FN
131/132," ilisema sehemu ya taarifa ya kampuni hiyo.

Taarifa hiyo ilisema safari za
ndege hizo zimesimamishwa
kuanzia Aprili 18 hadi Juni 30
mwaka huu na kuwa abiria
ambao walikwishakata tiketi
watarejeshewa fedha zao.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad