Ninalaani vikali udhaifu wa Kiti cha Spika na aibu ya Taifa letu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Tunachoshuhudia Bungeni siyo demokrasia kazini, bali domoghasia kazini. Ninalaani vikali udhaifu wa Bunge (Spika na Naibu wake), upendeleo, na lugha za kihuni za baadhi ya wabunge (wa vyama vyote) ambazo zinatufanya tuhoji kama wabunge wetu wako kutunga sheria na kusimamia serikali au wako kushindanisha nani analugha kali zaidi Bungeni.

Tunachoshuhudia Bungeni kinapaswa kisababishe maswali kwa wapiga kura kama watu hawa walioko Bungeni wanastahili kuwepo Bungeni na wapiga kura wachukue uamuzi gani dhidi yao ufikapo uchaguzi Mkuu au hata kabla. Kuendelea kuvumilia udhaifu huu wa chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi ni kuendelea kuvumilia udhaifu wa utawala wetu ambapo watu wanataka sifa kwa kuzungumza siyo kwa kutenda.

Spika Makinda na Ndugai wameshindwa kuongoza Bunge na sasa wanaburuza. Mpaka pale kiti cha Spika kitakapoacha upendeleo wa chama chao ndio Bunge litaongozwa kwenye misingi haki, usawa, heshima na utu. Kila mmoja akitambua wajibu wake na kwa wenzake ndio Bunge litasimama na kufanya kazi yake ya kuwawakilisha wananchi, kusimamia na kushauri serikali lakini zaidi sana kutunga sheria zenye matokeo bora kwa wananchi na mfumo wetu wa utawala.

Tunapoangalia Bunge sasa tunashuhudia udhaifu ukipewa kiti cha enzi, uzembe ukivishwa kilemba na uhuni ukishangiliwa. Tunashuhudia aibu ya taifa letu mbele ya watoto wetu. Nalaani vikali yote hayo!!

MMM

NB: Kama na wewe unajisikia kulaani vikali tuliyoyashuhudia hadi hivi sasa gonga "like" au/na andika kuunga mkono msimamo huu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukimchukua chizi wa hapa mirembe ukampa uspeeker anaweza kufanya vema kuliko huyu dem Anne.. Anadhihirisha kuwa madem hawawezi kuwa viongozi kabisaa.. Wa2 wanatukana km wapo kwenye kilabu cha komoni na speeker amekaa anatizama tu! Tatizo uspeeker wa promo so lazima awaridhishe waliompromoti asije akapigwa chini ujumbe wa halmashauri kuu..

    ReplyDelete
  2. Tumeshawajua, watakuja tu 2015.

    ReplyDelete
  3. IWAPO HAO VICHAA WALIOFUKUZWA BUNGENI NDI WATAPEWA NCHI HAKUNA TOFAUTI NA SYRIA HAKUNA CHA KUJIFUNZA KA KIZAZI CHA UTANDAWAZI KILICHOLELEWA NA BEKITATU KILICHOKOSA MALEZI YA WAZAZI "KWENYE MTANDAO SOMENI 'UTANDAWAZI NA MALEZI'WAJENZI WA DUNIA' MUTAONA KWANINI BUNGENI MAADILI YAMEPOROMOKA SIO KILA MWENYE COGNITIVE ABILLITY BAS AMEELIMIKA WAKATI AFFECTIVE NA PYSCHOMOTOR UKO POOR HUFAI KATIKA JAMII YOYOTE

    ReplyDelete

Top Post Ad