Shilole na Q-chief Kunani? Wanaswa kwenye Mapozi Tata Ndani ya Ndege

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na muimba Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’  hivi karibuni waliawaacha midomo wazi wasafiri ndani ya ndege kufuatia tukio lao la kufanya ‘malavidavi’ bila kujali.

Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.
Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.

“Tunakubaliana na kazi zao, lakini kusema ule ukweli, sisi abiria wenzao tulishangaa sana, unajua kuonesha vitendo vya mahaba ndani ya ndege si utamaduni wetu Wabongo,” alisema abiria huyo aliyekuwa akienda Mwanza kikazi.
Aliongeza kuwa, ilifika mahali baadhi ya abiria walitaka kuwafungukia ukweli kwamba wanachokifanya si adabu hasa ikizingatiwa kuwa wao wana majina makubwa katika burudani za Bongo.
Kufuatia taarifa hizo na kudakwa kwa picha zao, Amani liliwasaka watuhumiwa hao kila mmoja kwa wakati wake ili kusikia kutoka kwao juu ya kufanya madudu ndani ya ‘pipa’.

Kwa upande wake, Shilole alisema kuwa mabusu ni vitu vya kawaida kwake ikizingatiwa Q-Chillah ni mwanamuziki mwenzake kwa hiyo hakuna tatizo.
“Jamani kwani mabusu yana shida gani, yule (Q-Chillah)  ni mwanamuziki mwenzangu na tumezoeana. Yale yalikuwa ni mambo ya kawaida tu na utani, si vinginevyo,” alisema  Shilole.
Q-Chillah simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokelewa, lakini baadhi ya watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo hana kawaida ya kupokea simu kama namba hazijui. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wamekutana wote malimbukeni wa mapenzi Mtu Na heshima zako uwezi kufanya maambo ayo tena mbele ya kadamnasi ya Watu kweupepeee

    ReplyDelete

Top Post Ad