Alitaka mimba itolewe sasa anadai mtoto kisa ni wa kiume.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii imemtokea binamu yangu, akiwa University alikuwa na boyfriend, mapenzi ya ujana na ahadi za kuona, ikatokea binamu alipata ujauzito, akiamini yuko kwenye strong relationship, akamumbia jamaa. Du kusikia habari hiyo jamaa aliomba mimba itolewe na wamalize shule, waanze kazi ndio wafanye mipango ya ndoa. Binamu yangu hakutaka kuitoa ile mimba, tumbo lilivyoanza kuonekana, basi wazazi wake ilibidi wamuulize, aliwaieleza ilivyokuwa, baba yake ambae ni mjomba wangu alikuwa mkali sana kwasababu binamu yangu kwa akili za darasani alijaliwa.

Wazazi waliamua kumsaidia mtoto wao, wakampa support yote, alijifungua salama mtoto wa kiume, na wazazi walimchukua mtoto yule akiwa na miezi mitatu, ili binti yao aendelee na masomo. Binamu yangu alimaliza shule na matokeo mazuri sana, alipata kazi, akajiendeleza zaidi na shahada ya uzamili. Hakupata bahati ya kuolewa lakini anamudu kumsomesha mtoto wake katika shule nzuri tu, na maisha yake na mtoto wake ni mazuri sana.

Kijana alitoka kwenye familia nzito, zengwe lilivyotokea, wazazi walimtafutia shule nchi za mbali, akakata mawasiliano na binamu yangu kabisa. Dunia ni duara, amekutana na baba wa mtoto, alimaliza shule na kuoa, yeye na mkewe wamebahatika kupata mabinti wawili, sasa kujua mtoto wa kiume aliye nae ni yule wa binamu yangu tu, anamsumbua sana kutaka mtoto wake, tena kwakuwa binamu yangu hana mume, anajiona anahaki ya kwenda kwake saa yeyote ile. Mpeni ushauri binamu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo ndg yako aache ufala

    ReplyDelete
  2. Ushauri gani,mambo mengine ni kutumia common sense,akijilegeza imekula kwake na atakuwa fala sana

    ReplyDelete
  3. mimi ushauri wangu ni huu mtoto ameshazaliwa na aliyemgaramia mtoto mpaka akakuwa ni wazazi wa binti kwa nini huyu anayeomba ushauri asiombe kwa wazazi wake ambao ndio wamemlelea huyo mtoto wakati binti yao akisoma hapa sijui imekakaaje hii au wazazi wa binti hawapo hai anyway mimi ushauri wangu ni huu baba ni baba tu siku zote haijalishi amemlea au vipi huyu mwenye kutaka mtoto wake alipe garama zoote kuanzia mtoto alipo zaliwa mpaka sasa akishalipa anaweza kumchukua mtotowake kwa maelewano lakini hili jambo liende mbele ya sheria maana sheri ni msumeno ni hayo tuasikubali amchukue kirahisi

    ReplyDelete
  4. mimi ushauri wangu ni huu mtoto ameshazaliwa na aliyemgaramia mtoto mpaka akakuwa ni wazazi wa binti kwa nini huyu anayeomba ushauri asiombe kwa wazazi wake ambao ndio wamemlelea huyo mtoto wakati binti yao akisoma hapa sijui imekakaaje hii au wazazi wa binti hawapo hai anyway mimi ushauri wangu ni huu baba ni baba tu siku zote haijalishi amemlea au vipi huyu mwenye kutaka mtoto wake alipe garama zoote kuanzia mtoto alipo zaliwa mpaka sasa akishalipa anaweza kumchukua mtotowake kwa maelewano lakini hili jambo liende mbele ya sheria maana sheri ni msumeno ni hayo tuasikubali amchukue kirahisi

    ReplyDelete

Top Post Ad