BUNGENI: Vurugu zasababisha Bunge kuahirishwa hadi jioni.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cuf kuwa ni chama cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni, wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...

Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge..

Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.

Hiki ni Kipande cha hutuba hiyo ambacho nimekitoa Jamii Forums:
"Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo "
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Cuf wanachukia bila kufikiri kwa kina coz Wenje yuko bayana

    ReplyDelete
  2. Hakuna jipya..

    ReplyDelete
  3. Wanachukia nini,na sera zao zinaelekea kwenye ushoga,usagaji,useless party with hopeless leaders!

    ReplyDelete
  4. watanzania kuweni na upevu mkubwa wa kufikiri abari iliyo tolewa ipo sawa kabisa. ila wapokeaji awajapokea kwa umakini na wengi wenu watanzania mnapokelea jambo kwa ushabiki na sio nia ya kutaka kufahamu mm naelewa kwanini chadema wanasema hivi kila chama kina taratibu zake jiulizeni ni kwanini wamesema awajakurupuka kusema hivyo ni mada iliyo andaliwa kama aina ukweli basi aipo mbali na ukweli. naishi ulaya sasa ni zaidi ya miaka 5 ukitembelea baathi ya makumbusho vipo vitu vingi sana toka Tanzania wapo chura wa Shaba wametolewa Tanzania imeandikwa chura hawa asili yake ni Tanzania. je ulaya ni Tanzania? jiulizeni maswali hayo then achene ushabiki tafuteni kuelewa.

    ReplyDelete
  5. WENJE FANYAKAZI MAANA UKOMBOZI WA NCHI NI GHARAMA SANA,WATAKAZANA KUPINGA LAKINI WATA ELEWA BAADAYE NINI ULICHO KUWA UNAKISEMA!

    ReplyDelete

Top Post Ad