Chui Amng'ata Rais wa Botswana Khama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Botswana, Ian Khama ameshonwa baada ya kung'atwa na Duma, kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini humo.

Mnyama huyo alikuwa analishwa alikokuwa anahifadhiwa katika kambi ya kijeshi wakati alipomrukia rais Khama na kumgwara

Tukio hilo ilikuwa ajali tu wala sio shambulio kali, kwa mujibu wa msemaji wa serikali Jeff Ramsay aliyezungumza na waandishi wa habari.

Majeraha ya Bwana Khama, yalikuwa madogo wala haikujitokeza kama ajali kubwa.

Inaarifiwa ajali ilitokea ghafla na kumgutukia Rais Khama na walinzi wake.

"Duma alimgwara tu lakini sio kumshambulia, kama wanavyodahani watu wengi,'' alisema bwana Ramsay.

Bwana Khama alionekana akiwa amevalia plaster kwenye mkutano ulioandaliwa baada ya tukio hilo.

Duma, ambao ndio wanyama wenye kasi kubwa zaidi ardhini, ni moja ya wanyama wanaokabiliwa na tisho kubwa la kuangamia.

Ni wanyama 12,400 pekee wanaosemekana kusalia mbugani katika baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Botswana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad