Diva Loveness Aweka Tofauti Pembeni Aamua Kumsuport Boss Lady Big Brother Africa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Juzi (May 26) ndio ulifanyika ufunguzi rasmi wa shindano kubwa Africa la Big Brother ambalo mwaka huu limepewa jina la “The Chase”, na tayari washiriki wa nchi zote ikiwemo Tanzania wamekwisha fahamika.

 Huddah Monroe a.k.a The boss lady ambaye ni model mwaka huu ndio amebeba imani za wakenya za kurudi na kitita cha $300,000 zinazoshindaniwa katika msimu wa 8 wa shindano la Big Brother “The Chase” baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo ya jirani.

Siku chache zilizopita jina la Huddah limeonekana kupata umaarufu zaidi Tanzania hasa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya binti huyo mwenye historia ya matukio mengi ya utata huko Kenya (pamoja na kujihusisha na upigaji wa picha za utupu) kujikuta anaingia katika ugomvi wa maneno na mtangazaji maarufu hapa Tanzania Loveness Love a.k.a Diva kutokana na kinachoaminika kuwa sababu ni Prezzo.

Diva a.k.a mimi Kupitia akaunti yake ya twitter, juzi (May 26) aliandika tweet inayoonesha kuweka kando tofauti alizokuwa nazo na Huddah na kuahidi kumsupport kwa kutokumwandikia “shit” kama njia ya kumuunga mkono “wifi” katika BBA.
Diva amekuwa akidai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper kutoka Kenya CMB Prezzo, kitendo kilichopokelewa tofauti na mrembo Huddah ambaye pia kulikuwa na tetesi aliwahi kudate na “Liq Her” hit maker, Rapcellency, Prezzo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad