Exclusive: Linah na Barnaba waeleza kwanini hawatakuwepo kwenye ’13 Years Anniversary in Music’ ya Jaydee

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo.

Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo.

“Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”

Kwa upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine.

Hata hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee. “Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri,” amesema Barnaba.

Credits:Bongo 5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Au nyie lina na barnaba mameneja wenu ni akina ruge na wenzake ambao wana bifu na jd? Acheni hizo bhana

    ReplyDelete
  2. mkumbuke nanyinyi mtamhitaji oooh hooo haya nyi mbanieni.

    ReplyDelete
  3. ukweli ni kwamba nyie mko chini clouds fm..mnafata maarisho yakina ruge na kusaga..mnaogopa kuxhuxhwa kimzik..

    ReplyDelete
  4. Hahahaha dunia na vituko vyake kila kukicha

    ReplyDelete
  5. habari ndio hiyo watoto wa ruge hao na mtakufa maskini kutokana na ufinyu wenu wa mawazo

    ReplyDelete
  6. Mnamuogp ruge nyinyi mbwa koko

    ReplyDelete
  7. Sio ishu dada hata peke yako unalisongesha JOTO HASIRA kaza but tupo nyuma yako.

    ReplyDelete
  8. HuoNdo ukweli hao madogo wako chini ya ruge na kusaga so hawawezi kuungana na jide. But sio issue mama jide ww kiboko unaweza kuwakimbiza cc tupo tutakupa sapot mama!!

    ReplyDelete

Top Post Ad