Hatimaye TFF yapanga Tarehe ya Uchaguzi kutekeleza Agizo la FIFA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) utafanyika Septemba 29 mwaka huu, ikiwa ni kutekeleza agizo la Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa).
Uamuzi wa kufanya uchaguzi huo Septemba 29 ulifikiwa Dar es Salaam jana baada ya kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Leodegar Tenga.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Februali 24 mwaka huu, lakini Fifa iliufuta na kuagiza mchakato uanze upya baada ya kubaini kuwapo na kasoro kadhaa.
Mbali ya kuagiza mchakato uanze upya, Fifa pia iliiamuru TFF iunde kamati ya maadili ya ngazi ya mwanzo wa uchaguzi na rufaa.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Tenga alisema kuwa, kamati ya utendaji imepokea maagizo ya Fifa na imekubali kuyatekeleza bila kipingamizi.
“Tumepokea maagizo ya Fifa yanayotuelekeza cha kufanya, siyo TFF wala mtu mwingine yeyote anayeweza kuongeza jambo lingine.
“Tunatakiwa kuunda Kamati ya Maadili, Kamati ya Rufani ya Maadili, kufanya marekebisho ya Katiba, mchakato mpya wa uchaguzi, waliokuwapo na wapya waruhusiwe. Tumejitahidi kuhakikisha uchaguzi uwe kabla ya Oktoba 30 mwaka huu kama Fifa walivyotuagiza,” alisema Rais Tenga.
Tenga alisema notisi ya mkutano mkuu wa dharura itatolewa Juni 12 au 13, wakati Juni 15 Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kwa ajili ya kupokea mapendekezo kabla ya kuyapeleka tena Fifa.
Kamati itakutana Julai 14 na 15 na kuunda Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad