Jack Wopler na Baby Madaha Ndani ya Beef Zito, Madaha Aapa kuto ongea na Wolper

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
Akizungumza na Ijumaa, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.

MADAI YA MADAHA
“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”

HUYU HAPA WOLPER
Wolper alipotafutwa na Ijumaa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.
“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad