Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


    Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

    Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

    Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

    Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

    Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad