Magufuli Akumbwa na Kashfa Nzito!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii imetoka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani. Sehemu hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha kwenye wizara iliyooko chini ya Dr John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Spika,baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi bilioni 95 na kupelekwa wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi bilioni 252.975 katika kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge kuhusiana na suala hili kwani kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka husika wa fedha kuhusiana na kifungu hiki alisema, naomba kunukuu “malipo ya madeni ya mwaka wa nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la mradi usiohalisi hs.252,975,000,000.

Miradi katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya madeni ya miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba hii sio halisi” (chanzo: taarifa ya CAG uk.160,fungu 98)

Mheshimiwa Spika,fedha hizi “zilizopotea”au “kulipwa kifungu hewa” ni sawa na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya barabara ifuatazo kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014;

i. Barabara
ya Usagara-Geita-Kyamyorwa
(KM 422)

ii. Barabara
ya Kigoma-Kidahwe-Uvinza-
Kaliua-Tabora (KM 443)

iii. Barabara
ya Nangurukuru-Mbwemkulu
(KM 95)

iv. Barabara
ya Sumbawanga-Matai-Kasanga
Port (KM 112)

v. Barabara
ya Manyoni-Itigi-Tabora (KM264)

vi. Barabara
ya Tabora-Ipole-Konga-Mpanda
(KM 359)

vii. Barabara
ya Kidatu-Ifakara-Lupilo-Malinyi-
Londo-Lumecha/Songea(KM-
396)

viii. Kuondoa
msongamano barabara za Dar
(KM- 102.15)

Aidha, ni sawa na kusema kuwa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 316.218 imepotea kwa kutumia mahesabu ya wizara ya ujenzi kuwa kilomita moja ya lami inajengwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nane (800,000,000), hii ni sawa na kusema kuwa barabara ya kutoka Manyoni-Itigi-Tabora (KM 264) Changanya na barabara ya kutoka Chunya – Makongorosi (KM 43) na Barabara ya Tangi Bovu –Goba (KM 9), zimepotea kutokana na ufisadi huu.

Chanzo: hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa msaada Marcossy Albane.

Source:JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad