Mchezaji wa Chelsea Adam Nditi na Sakata lake la Kuichezea Taifa Stars

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nditi ambaye alizaliwa Zanzibar mwaka 1994 kabla ya kujiunga na timu ya Chelsea U13 miaka kadhaa iliyopita baada ya kuhamia England na familia yake, katika siku za hivi karibuni ameibuka kuwa mjadala mkubwa suala lake la kuichezea timu ya taifa ya Tanzania.

Siku za nyuma shirikisho la soka nchini TFF liliwahi kutoa ripoti kwamba walijaribu bila mafanikio kuweza kumpata Adam kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza lakini hawakufanikiwa – ingawa Adam Nditi mwenyewe anakanusha hakuwahi kupokea taarifa yoyote kutoka kwa TFF wala ubalozi wa Tanzania UK kuhusu suala la kuja kuichezea Tanzania.
Kwa upande wa baba yake ya Nditi, aitwaye Eric Nditi amesema yeye kama mzazi wa mchezaji huyo hayupo tayari kumruhusu mtoto wake kuja kuitumikia Taifa stars mpaka pale taratibu zote zitakapofuatwa. “Kiukweli kabisa kama taratibu zote hazitofuatwa Adam hatokwenda Tanzania kuichezea timu ya taifa. Sitokubali mwanangu aende Tanzania kwa taarifa za magazetini, kiutaratibu ili mchezaji aitwe kwenye timu taifa inabidi benchi la ufundi la timu husika lijilidhishe na kiwango cha mchezaji na sio kumuita tu bila kumfanyia scouting, pia inabidi mchezaji atumiwe taarifa rasmi,” anasema Nditi.
Pia Eric Nditi amesikitishwa sana na taarifa kwamba mwanae hataki kuichezea timu ya taifa ya Tanzania. “Tatizo la nchi yetu siasa zipo kila mahala, bora wewe Shaffih umekuja mpaka huku kujua ukweli. Adam ni mtanzania wa kuzaliwa na kukulia kwenye nchi hiyo na yupo tayari kuichezea nchi yake ikiwa atatakiwa na mwalimu. Napenda kuona anaisadia nchi yake lakini kwa utaratibu unaoeleweka.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad