Mke wa Mshikaji Wangu Aniduwaza!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jana nimeduwazwa sana baada ya mke wa rafiki yangu kunitamkia wazi kuwa ananipenda na anataka kutoka na mimi.
Tangu nifahamiane naye miaka takribani mitano sasa tumekuwa tukiheshimiana naye sana kama mashemeji. mwaka huu akaniambia kuwa mumewe ameanza kubadilika kwa kuzidisha ulevi, kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kulala nje na pia alizifuma meseji za mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa mtu aliyemsave kwa jina la kiume, hivyo nimsaidie kumshauri ili abadilke ila akanionya nisimwambie kama ni yeye ndiye kaniambia.

Nilimtia moyo kuhusu hali hiyo na kumwomba awe mvumilivu na asichoke kuongea na mumewe kuhusu hali hiyo ili abadilike. Binafsi nilipata wakati mgumu wa namna gani nitamshauri jamaa bila kumtajia makosa yake na wapi nimeyapata hivyo nikashindwa hiyo kazi.

Mke wa jamaa akaanza kunipigia simu usiku kulalamika kila mumewe anapochelewa kurudi na wakati mwingine akinipigia alfajiri kuniambia kuwa mumewe hajarudi hadi muda huo. Niliendelea kumtia moyo ingawa mambo hayo yalikuwa ni ya kweli.

Cha ajabu kuanzia wiki jana amekuwa akinitumia meseji za mapenzi, nikajua ni hizi meseji ambazo watu hutumiana hivyo sikujali sana hadi pale aliponiandikia akiniambia kuwa yuko serious anataka kutoka na mimi. Sikuamini nikampigia simu kusikia sauti yake kama ni yeye kweli, ndipo aliponithibitishia kuwa yuko serious na atatunza siri na kunitunzia heshima yangu kwa jamaa kwani tayari moyo wake umeangukia kwangu.

Sikuweza kumjibu kitu kwa namna nilivyopatwa na mshangao. hadi sasa anaendelea kunibembeleza na kunipa mbinu nyingi za kutimiza lengo lake bila kujulikana na watu.

Binafsi sina lengo la kumsaliti mshikaji wangu ila nimelileta kwenu ili mnishauri nimjibu vipi huyu mwanamke ili heshima yangu kwa familia hii iendelee kuwapo na pia kusitokee chuki yoyote kutokana na kadhia hii itakayopelekea urafiki wangu na familia hii kuyumba au kupotea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. dah yahitaji moyo mkubwa weka tamaaa nyuma tumia busara mkubwa,ingawa vijana wa siku izi angeona ni DONDOKELA{MCHEKEA}.

    ReplyDelete
  2. Dah,mjomb huo mtihan! Ila nachokuomb we kaza uckubal xab ht km mshkaj wake anamakosa co iwe njia ya ww kukubal kirahc,utagombn namshkaj wako ksa madem hao wapo2.

    ReplyDelete
  3. Kula tu ila usizoee

    ReplyDelete
  4. penzi ni kikohozi. achana nae. hana mapenzi lolote ni hasira tu hizo. na ukitoka nae jua haitokua siri hiyo. hakuna siri ya wawili hata siku moja.

    ReplyDelete
  5. mtaongeza chain.. Yawezekana kuna maambukizi hapo.. Kaa mbali!

    ReplyDelete
  6. Hayo ni mabango achana naye

    ReplyDelete
  7. Duh mpe moyo tu lakin ucjaribu ku do utakuwa umekosea sana..... Pole kwa mtihani huo

    ReplyDelete
  8. achana nae malaya tu huyo anataka kukugombanisha na mchizi wako

    ReplyDelete
  9. achana nae,huyo muhuni,kama alivo kutongoza wewe. na wengine anaweza kwenda nae,na huyo rafki yako, je kama ana ukimwi?utambukizwa ufe.usiende tena badilishanamba ya simu.

    ReplyDelete
  10. Msulubu kaka halafu sepa kimtindo kama vip, mtoto asikuone bwege flani

    ReplyDelete
  11. May 24, 2013 at 5:44 AM hapo umesem kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad