Real,Maurinho chali Bernabeu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndoto ya kocha Jose Mourinho na Real Madrid kusaka taji la 10 la Ligi ya Mabingwa imezimika pamoja na kushinda 2-0, lakini Borussia Dortmund imefuzu kwa fainali kwa  jumla ya mabao 4-3 jana kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Wakati  Real wakifunga virago jana ndugu zao Barcelona leo watakuwa na kibarua kizito mbele ya Bayern Munich baada ya kunyukwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza na kutoa uwezekano wa kuchezwa fainali ya kwanza inayowakutanisha Wajerumani pekee.
Mshambuliaji Karim Benzema aliingia akitokea benchi na kuifungia Real bao la kwanza katika dakika 82 akimalizia pasi ya Mesut Ozil kabla ya Sergio Ramos kupachika bao la pili kwa shuti la karibu baada ya kupokea pasi ya Benzema.
Real watajilaumu wenyewe baada ya washambuliaji Cristiano Ronaldo, Gonzalo Higuain na Ozil kupoteza nafasi tatu za wazi za kufunga wakiwa wao na kipa Dortmund, Roman Weidenfeller.
Dortmund walipata pigo katika dakika15 baada ya kiungo wake Mario Gotze kuumia na kutoka nje nafasi yake kuchuliwa na Kevin Grosskreut.
Utamu wa mchezo huo ilikuwa ni vita baina ya beki wa Real, Ramos na mshambuliaji Robert Lewandowski wa Dortmund aliyeweka rekodi ya kufunga mabao nne katika mechi moja ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wiki iliyopita.
Katika dakika 48, Lewandowski alikosa bao baada ya shuti lake kugonga mwamba na kurudi uwanjani, kipa wa Real, Diego Lopez alifanya kazi nzuri kwa kuokoa mashuti ya Reus na Pisczek katika dakika ya 61 na 64.
Kocha Jose Mourinho aliwapumzisha Fabio Coentrao, Gonzalo Higuain na  Xabi Alonso na kuwaingiza Karim Benzema, Kaka na Sami Khedira waliobadiliko mchezo wote kabisa kwa wenyeji.
MUUJIZA
Barcelona wanahitaji mzuka wa Deportivo La Coruna kuweza kubadilisha matokeo ya mabao 4-0 waliyofungwa na Bayern Munich leo watakapokuwa nyumbani katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa.Deportivo La Coruna iliwashangaza wengi kwenye michuano hiyo msimu wa 2003-04, wakati walipoichakaza AC Milan 4-0 katika mchezo wa marudiano na kuwafungasha virago kwa jumla ya mabao 5-4.
Mshambuliaji wa Uruguay, Walter Pandiani alifunga bao la kwanza katika dakika tano kwenye usiku ya kumbukumbu uwanja wa Riazor, wakati La Coruna ilipoiduwaza Milan iliyokuwa na nyota kama Paolo Maldini, Kaka na Andriy Shevchenko.
Pandiani anaamini Barca pia inahitaji bao la mapema kama kweli wanataka kucheza fainali jijini London kwenye Uwanja wa Wembley.
“Kufunga bao la mapema katika mechi ni hatua muhimu ya kuwafanya wachezaji kujiamini zaidi,” alisema Pandiani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad