STL na mchekeshaji Churchill wa Kenya Leo kuperform kwenye ufunguzi wa Big Brother Africa “The Chase”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Yakiwa yamebaki masaa machache kabla lile shindando kubwa la Big Brother Africa ambalo kwa mwaka huu limepewa jina la “The Chase” kuzinduliwa rasmi leo (May 26) nchini Africa Kusini, tuna hakika tayari mashabiki wanajiandaa kwa kuhakikisha wamelipia decoder zao.

Wasanii wanaotegemewa kushiriki Katika ufunguzi wa reality show hiyo kubwa Africa hiyo kesho ni pamoja na rapper wa kike wa Kenya mwenye makazi yake nchini Uingereza kwa sasa (baada ya kuishi Norway kwa muda mrefu) Stella Mwangi aka STL ambaye ataongozana na mchekeshaji maarufu wa Kenya, Churchill.

Wasanii wengine wanaotegemewa kuperform katika show hiyo ya ufunguzi ni Mafikizolo kutoka Africa Kusini, Don Jazzy, D’Prince na Wande Coal kutoka Nigeria.

Housemates 28 wanaowakilisha nchi mbalimbali za Africa ikiwemo Tanzania, wanategemewa kujulikana katika show hiyo ya msimu wa 8 wa Big Brother Africa itakayoonekana live katika nchi zipatazo 50 za Africa kupitia Africa Magic, AfricaMagic Entertainment, AfricaMagic World, Dstv channel 197 and 198. pamoja na kurushwa live katika mtandao hiyo kesho Jumapili (May 26).


Mshindi wa BBA ‘The Chase’ anategemewa kuondoka na kitita cha $300,000 baada ya siku 91 za kukaa katika jumba hilo lenye raha za kila aina.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad