Ushauri mchumba wangu anatembea na lecturer wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mimi ni kijana wa kitanzania, najitokeza hapa mbele yenu kuomba ushauri kwa haya makubwa yaliyonikuta.

Nilianza chuo miaka mitatu iliyopita, nikimaanisha kwa sasa nipo mwaka wangu wa mwisho katika hii kozi ninayoichukua. Nilianza chuo bila kuwa na uhusiano wowote ule wa kimapenzi na msichana hapa chuoni kwa mwaka wote ule wa kwanza.

Hali hiyo ilibadilika baada ya kuingia mwaka wa pili, kwani kipindi hicho kukawa na mwaka wa kwanza wanaingia na bahati nzuri nikatokea kumpenda msichana mmoja mrembo wastani sema ni mstaarabu haswaa. Nilijaribu bahati yangu na mungu si athumani huyu msichana akanikubalia na tukaanza mahusiano yeye akiwa mwaka wa kwanza,mimi wa pili. Tuliishi kwa amani na  furaha kwa kipindi chote kile(nikimaanisha semester zote mbili za mwaka wangu wa pili).

Kinachonifanya kuandika hapa ni hiki sasa, mwanzoni mwa semester iliyopita nilianza kusikia tetesi kutoka kwa marafiki zangu ya kuwa huyu msichana niliye naye anatoka na mmoja wa ma-lecturer wanaomfundisha. Sikuliamini hilo, nikaamua kumuliza mwenzangu kwamba nimesikia hili na hili, je kuna ukweli wowote? Alikataa kata kata na kusema huo sio ukweli na nisiamini kila ninalolisikia, kwa kuwa ni mstaarabu sana na kwa jinsi alivyokuwa akiongea basi nikamuelewa kwa muda ule.

Ila sikuishia hapo nikaendelea na uchunguzi wa chini chini bahati mbaya sikuambulia lolote kuhusu uhusiano wake na  huyo lecturer zaidi ya yeye kuwa na ratiba ya  kwenda kwao kila baada ya wiki mbili kuanzia ijumaa jioni mpaka jumapili ambao ni utaratibu wake toka anaanza chuo. Na hiyo ijumaa mpaka jumapili akiwa nyumbani mawasiliano yalikuwa yakipungua sana kwa sababu alikuwa akisema anakuwa busy sana na shughuli za nyumbani kwao na hata usiku ukimpigia simu alikuwa hapokei kwa madai analala na ndugu yake na kwahiyo atakuwa anampigia kelele.

Leo mchana sasa, nilimpigia simu twende tukapate chakula cha mchana lakini alikataa na kuniambia kuna kazi anaifanya kwanza mpaka aimalize ndio ataenda kula, mimi nikatangulia kwenda kula ila wakati narudi nikakutana na rafiki yangu, akaniuliza mbona nimekutana na bibie(mchumba wangu) anakula na Mr. X (huyo lecturer niliyeambiwa anatembea naye ) sehemu flani(ma-lecturer wengi ndio wanapokula hapo na kama utakuta wanafunzi basi ni mmoja mmoja ambao wako vizuri sana kifedha)… sikuamini, nikaenda kuhakikisha… Nilichokiona aisee sikuamini macho yangu, wote wawili walikuwa wamekaa wakipata lunch tena wakionekana wenye furaha.

Nilimpigia simu lakini hakupokea, aliishia kuiangalia tu simu yake na kuirudisha kwenye meza… Nikamtumia meseji ya kwamba nimemuona na nimezima simu yangu mpaka sasa, hapa natafakari nimfanyaje huyu msichana kwa hili alilonifanyia??? It hurts kwa kweli ikizingatiwa huyu lecturer ana mke kabisa so what if ndio tabia yake hiyo kutemebea na wanafunzi? Si  ndio kuambukizana magonjwa huku??

Naombeni ushauri wenu , nimfanyeje huyu kiumbe??
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. pole ndg yng bt ucpate tabu sn coz hao ndo walivyo,kwao kilichoko machoni ndo bora. Ictoshe hujawahi kumtambulisha om,ucwaze we kula tu kitabu wanawake mbn wko wengi tu!

    ReplyDelete
  2. Mburura we we,SOMA utadisco kwa ajili ya kipoch manyoya

    ReplyDelete
  3. jus continue with your life n studies though u got hurt so much
    there is six billion people around d world dont ruin ur present yl u can have beautiful life ahead of you

    ReplyDelete
  4. Endelea kula kitabu 2 achananacho hicho kiruka njia kitakupotezea muelekeo buure!.

    ReplyDelete
  5. achana nae maana ni msaliti tia msul kwenye kitabu

    ReplyDelete
  6. Study get yo own cash then kna dada watakuj kbao....
    wazur zaid na weny heshma na wastaarabu...
    Shit hapenz!!! Drop it then move on...
    yu ar a man...n us man....we got standard n mcmamo...2pa kule broda

    ReplyDelete
  7. Just study my dear, to get a faithful girl in chuo noi vigumu sana so I advise you to just continue with your studys cause there is still time for you ahead. Just study and build your life. Let her go. She will come back to you when ts late but all in all just move on. You don't know wamefanya nini? Either huyo mwalimu anaeza akakufanyia mbaya... Just muv on even though it will hurt but just be strong.

    ReplyDelete
  8. HAYO NI MAPITO BRO, KUPENDA SIO MKATABA WA MAISHA ENDAPO HAUPENDWI, JILINDE WEWE NA MAISHA YAKO, HUYO HAKUPENDI ANA MPANGO WA KUKUANGAMIZA, USIWE KING'ANG'ANIZI HATA KUNG'ANG'ANIA MOTO, BADO UNA MAISHA MBELE, UTAPATA YULE ALIYETOLEWA KWENYE UBAVU WAKO SI NDONDOCHA HUYO. THINK BIG, ACT MANLY, ADORE YOUR FUTURE, MAKE RIGHT DECISION, LET HER GO TO HELL 4GET UR PAST, PLAN UR FUTURE, LIFE GOES ON. JUSTUS UDOM

    ReplyDelete
  9. Kwanza pole sana,huyo Binti achana nae shida yake sio kama anampenda huyo lecture anataka apasishwe mitihani ndio maana anaji sacrife utu wake!Wakina kihiyo wako wengi mmoja wapo ndio huyo binti.Ushaujua ukweli tulia soma utapata mwingine.

    ReplyDelete
  10. Ukimbie ukimwi,kwanza si mwaminifu na pili si mtu wa ndoa kwa ss anawaza wanaume wa kumtosheleza kwa mahitaji yake na hana mapenzi.Najua ni vigumu kukutoka bt kama uliweza kupenda kuchukia pia utaweza

    ReplyDelete

Top Post Ad