Wema Sepetu "Mimi na Wanaume tu, Siwezi Badilisha Hii Style"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wema ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Endless Fame, anadaiwa kuwa beneti na kijana aitwaye Robby lakini mwenyewe amesema kwamba hakuna anayeweza kumtenganisha na wanaume.
Habari zinasema kuwa, Wema na Robby wamekuwa wakipiga picha za kimahaba na mnyange huyo kuziingiza kwenye mtandoa wake na kumtambulisha kijana huyo kwa jina la ‘Honey’

Risasi Jumamosi lilifanya juu chini na kumsaka Wema ili kumtaka ajibu tuhuma za kuwa katika mahaba na kijana huyo.
Mei 22 mwaka huu, mwandishi wa gazeti hili alifika ofisini kwa mrembo huyo, Mwananyamala Komakoma jijini Dar es salaam na kumbana kwa maswali juu ya kuvuja kwa picha zake hizo akiwa na Robby na nyingine akiwa na wanaume wengine tofauti.
“Watu wamekuwa wakinizungumzia kila kukicha, tena maongezi yao yamekuwa yakianzia kwenye baadhi ya picha zangu, kila mtu ana namna ya kutengeneza ‘laifu’ yake na miye huwa sioni shida mwanaume asiye hawara yangu kunikisi au miye kumkisi,” alianza kujitetea.

“Ukifuatilia historia yangu mara nyingi utagundua marafiki zangu wengi ni wanaume kuliko wanawake na wengi wao wanakuja kwangu, tunakunywa na wanaondoka mida mibovu, kwa asiyenijua anaweza kuhisi ni mabwana zangu kumbe siyo, hata kwenye mitandao huwa sioni tabu kuweka picha za mtu akinikisi au nikimkisi,” aliendelea kusema.

“Siwezi kubadilika hii ni life style yangu. Siwezi kuacha kuwa karibu na marafiki wa kiume, hivyo ndivyo nilivyoumbwa watu wasinishangae, suala la kukutana na mtu na kupiga naye picha siyo ishu kwangu, ningekuwa mtu wa ajabu sana kama ningekuwa nawakisi midomoni au wao kunikisi mdomoni,” aliongeza.
Wema amesema kuwa watu wana hisia mbaya juu yake na Robby jambo ambalo siyo sahihi kwa kuwa, katika maisha yake anawapenda marafiki wa kiume zaidi ya wanawake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo wema ana pepo la ngono inabidi apepewe!!

    ReplyDelete
  2. Jamani nipeni namba yake napenda sana watu wenye pepo za ngono,nisaidieni waungwana

    ReplyDelete
  3. wema jaribu kujiweka mbali na hanasa za dunia,midomo ya wanaadamu si mizuri.utapata hasadi.usikubali kujifaharisha sana,msikize mama yako anavolalamika,jaribu ujistiri.wako wapi wasanii,wabunge,maraisi,wengi walikuwa wakubwa,baadae kifo kiliwajia.muogope mungu,urudi kwake.

    ReplyDelete
  4. yaah combaya km ni lyf style yako bt angalia jamii inakuchukuliaje sometymes we hv 2 change according to de enviroment

    ReplyDelete
  5. Ifike wakati ya mtu tumuachie mwenyewe, huyo ni m2 mzima, ajua atendalo

    ReplyDelete
  6. Wanamsema tu dada wawatu kwa kuwa mzuri tu basi na kumfutilia kwa nini watu wana wivu hivyo?malaya kibao hamuwasemi mmemwona wema tu ndio mwenye makosa kwa kuwa nyinyi sio mastaaa wivu uta wauwa

    ReplyDelete

Top Post Ad