KUNA WIZI UMETOKEA BENKI KUU
•••••••••••••••••••••••••••••• •••••
Jambazi "wote laleni chini pesa ni
za serikali na maisha ni ya
kwenu",wote wakalala chini
... HII INAITWA DHANA YA
USHAWISHI-kubadilisha njia ya
kawaida ya kufikiria
•••••••••••••••••••••••••••••• •••••••
Kuna dada kwa woga akawa
amelala chini kimitego,
Jambazi "dada embu kuwa na
adabu chukua kanga jifunike hili ni
tukio la ujambazi na sio la
ubakaji.
HUU UNAITWA WELEDI-zingatia
ulichofundishwa kufanya
•••••••••••••••••••••••••••••• •••••••••
Walipotoka kwenye wizi jambazi
mdogo ambaye ana shahada ya
uzamili ya biashara akamwambia
mwenzake,"tuzihesabu hizi
fedha,yule mkubwa akamcheka
kwa dharau na kumjibu,"wewe
mjinga sana hizo hazina haja ya
kuhesabu saa mbili watatutangazia
kwenye taarifa ya habari tumeiba
kiasi gani.
HUU INAITWA UJUZI-Sikuhizi ujuzi
ndio bora kuliko vyeti
•••••••••••••••••••••••••••••• •••••••••••
Baada ya majambazi kuondoka
meneja akamwambia mhasibu wa
bank, " ujumlishie na zile milioni
80 tulizo iba sisi".
HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA
MKONDO WA MAJI- kushabiihana
na mazingira magumu kwa faida
binafsi.
•••••••••••••••••••••••••••••• ••••••••••••
Mhasibu akafurahi na
kusema,"dah wizi ukitokea kila
mwezi itakuwa burudani sana.
HUKU KUNAITWA KUWA NA
MAWAZO CHANYA-Furaha ndio
kitu cha muhimu zaidi
•••••••••••••••••••••••••••••• ••••••••••••
Meneja kafurahi sana kwakuwa
sasa matatizo yake yametatuliwa
na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-
shikilia nafasi psle inapojitokeza
hata kama ni hatari kiasi gani
•••••••••••••••••••••••••••••• ••••••••••••
Haya usiku wake taarifa ya habari
ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana
wa millioni 100 umetokea leo
benki kuu,
Majambazi kuskia hivyo wakaanza
kuhesabu zila pesa lakini
wakajikuta na milioni 20 tu.
Yule jambazi mkubwa akashtuka
na kusema, "dah! yani meneja
kaiba mara nne zaidi yetu bila
kuchezesha msuli bora umeneja
kuliko ujambazi".
HII INAITWA ELIMU- ishike sana
elimu inanguvu kuliko dhahabu
•••••••••••••••MWISHO••••••••• •••••••