BEI YA BIA, SIGARA ZAZIDI KUPANDA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Serikali imeendelea kuongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi kama ambavyo kodi imekuwa ikifanya kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.
Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara pamoja na waagizaji magari watalazimika kutumia fedha nyingi zaidi ili kupata huduma hizo.
Vilevile baadhi ya bidhaa zisizokuwa za mafuta nazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi, ikiwamo mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara.
Vinywaji hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10. Kutokana na bajeti ya mwaka 2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh239 kwa lita moja.
Bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini ambayo haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita hadi Sh341, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita.
Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578, sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita. Kuhusu ushuru magari, umeongezwa kwenye magari yasiyozalisha na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.
Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara, huku ikiongeza mapato kwa Sh510 bilion
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli kwa hali hii serikali inapata kiasi kikubwa sana cha kodi, shida ni kwamba hazifanyi kazi iliyokusudiwa bali zinaishia mifukoni mwa viongozi na watoto wa vigogo. Tutakamuliwa kwa njia yoyote ile ilimradi vigogo serikalinini watimize malengo yao.

    ReplyDelete

Top Post Ad