DPP ASHINDWA KUMSHITAKI SUGU KUTOKANA NA MAPUNGUFU YA HATI YA MASHITAKA..... SUGU YUPO HURU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Dodoma Mjini, jana ilimuachia huru Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (41), maarufu kama Sugu aliyefikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya hati ya mashtaka kuonesha mapungufu.

Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama imeutaka upande wa mashtaka kurekebisha hati hiyo na kumfikisha tena mshtakiwa mahakamani huku Wakili wa Mbilinyi, Tundu Lissu akitaka kesi mpya itakayoletwa mahakamani iwe na maelezo ya Waziri Mkuu na awe tayari kusimama mahakamani kuthibitisha shitaka hilo.

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Elinaza Luvanda.

Awali akimsomea mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Harriet Lopa alidai kuwa Juni 24, mwaka huu, Mbilinyi akiwa Dodoma alituma ujumbe wenye lugha ya matusi kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Mshtakiwa alikana shitaka hilo. Hata hivyo wakili wa Mshtakiwa, Lissu aliomba kutoa hoja na kusema hati ya mashtaka ni mbovu na kuomba Mahakama itupilie mbali kwa sababu ina makosa.

“Lugha ya matusi haikutajwa, lugha gani hiyo ya matusi na hati ya mashtaka iko kimya, mshtakiwa atajitetea vipi,ataandaa utetezi namna gani kwani hata kinachodaiwa kuwekwa kwenye facebook hakijasemwa,” alidai Lissu.


Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali alisema kesi hiyo bado iko kwenye upelelezi na kutaka mshtakiwa aendelee na mashtaka yake mpaka itakapothibitishwa vinginevyo.


Kutokana na kauli hiyo ya wakili wa Serikali, Lissu alizidi kusisitiza hati ya mashtaka haina maelezo ya kutosha na inatakiwa kukidhi matakwa ya sheria.

“Hati ya mashtaka iliyoletwa si halali kinyume na kifungu cha 132 cha mwenendo wa makosa ya jinai na itakuwa makosa kama Mahakama ikikubali hati hiyo,” alisema.


Alitoa uamuzi wa Mahakama, Hakimu Luvanda alisema anakubaliana na maelezo ya Wakili upande wa utetezi Lissu kuwa hati hiyo ina mapungufu.

Alisema Mahakama inamuachia huru mshtakiwa na upande wa mashtaka unaweza kumshtaki tena mshtakiwa kama itaona umuhimu wa kufanya hivyo.

Akizungumza nje ya Mahakama Lissu alisema hati ya mashtaka dhidi ya Mbilinyi kuwa alitoa lugha ya matusi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda haijaeleza anachodaiwa kusema Mbilinyi.


Alisema Mahakama imetenda sawasawa kuifuta hati hiyo ilitakiwa ifafanue lugha ya matusi iliyotumika ni ipi. ”Hakimu hajasema Sugu hana makosa, lakini upande wa mashtaka ukajipange kutengeneza hati mpya,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. safi sana arudi mahakaman ye mlalamikaji!

    ReplyDelete

Top Post Ad