Exclusive: Jokate aongea baada ya Diamond kukiri kuwa anajuta kumkosea na kuuvunja moyo wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hivi karibuni Diamond aliamua kuweka ‘ego’ pembeni na kukiri kuwa Jokate Mwegelo ndiye msichana katika maisha yake aliyemkosea sana na anajuta kumuumiza
Diamond alifunguka hayo kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki iliyopita.

Akiongelea jinsi alivyomuumiza Jokate, Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea.”

Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”

Bongo5 imewasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond aliyesema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.

“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amesema Jokate.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daah mi naona maluwi luwi tu, issue hapa ilikuwa Joket aimsaliti Wema? Sio nani kamfuata nani jamani. Sasa ina maana shemeji alikuwa anasubiri waachana ili yeye ahamie? Khaaa wajemeni wasichana wa bongo njaa sana

    ReplyDelete
  2. Haipendezi cause wema na jokate wana share career zao na jokate alijua huyo buza kesha tembea na wema so angemtolea mbavuni hata kama alimfuata ila nahisi jokate alihitaji kick ambayo imemshusha in public

    ReplyDelete
  3. ama hakika watanzania tuna matatizo ya ufikiri; kweli habari za kijinga kama hizi mnaona ndo za kuuwekea umma kusoma ? tunajifunza nini na mambo kama haya yanasaidia vipi watanzania kutatua matatizo yao? fikiria na mfikiri acheni ujinga na kamwe mnaopost habri kama hizi mnachangia matatizo ya nchi hii kwa kiasi kikubwa sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Labda tukuulize huku kwenye title hii ya udaku umefwata nn kama nawe sio mshakunaku wakupenda. Matukio!! Kuna uhuru wa hii mitandao ya kijamii,hatuko sawa kifrika,tembelea JF au Michuzi kupata habari zaidi za kitaifa na uzipendazo,Mambo ya udaku waachie wadau wenyewe,kwa taarifa yako ni asilimia kidogo sana ya watz ndio wenyewe uwezo wa ku access haya mamitandao,fanya tafiti.


      Delete
  4. mhhhhhh ma sis huyo c mtu n kama mnyama xo msamehe ka vp

    ReplyDelete
  5. Nimefurahi Diamond alivyo ongea ukweli,atleast amemsafisha bint wa watu.amekua sasa

    ReplyDelete
  6. kama vp c mrudiane tu hamna talaka hapo..!!

    ReplyDelete
  7. Diamond siku zote penzi linauma acha penda penda maana kuna cku utapata cha moto pole sana Joketi lakini pia nawe kuwa makini maana unamfahamu vizuri Diamond

    ReplyDelete

Top Post Ad