google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html JAPO TULIFUNGWA ILA IVORY COAST HAWATA SAHAU-WATAJA WACHEZAJI WALIO KUWA MIBA KWAO | UDAKU SPECIAL

JAPO TULIFUNGWA ILA IVORY COAST HAWATA SAHAU-WATAJA WACHEZAJI WALIO KUWA MIBA KWAO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KIUNGO bora wa Afrika aliyecheza mechi zaidi ya 100 Barcelona tangu mwaka 2007 kabla ya kwenda Manchester City ameona mchezaji mmoja tu wa Taifa Stars.
Mechi baina ya Taifa Stars na Ivory Coast imeingiza Sh 502 milioni huku mashabiki 57,203 wakiwa wamelipa tiketi kuona mechi hiyo.
Yaya Toure, ambaye mwaka 2009 alikuwamo katika kikosi cha Barcelona kilichoweka rekodi ya kutwaa makombe sita tofauti, amemtaja Kelvin Yondani kama mtu aliyekuwa akimnyima raha uwanjani na kwamba anachelewa kwenda Ulaya.
Lakini, Gervinho na Solomon Kalou nao kila mmoja wamewataja wachezaji wao waliowasumbua na wanaodhani wanastahili kucheza Ulaya.
Mastaa hao ambao walikuwa na ulinzi mkali wa mabaunsa wa Ivory Coast walizungumza na Mwanaspoti kwa kina baada ya mechi ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Taifa Stars jijini Dar es Salaam huku kila mmoja akitikisa kichwa mwisho wa siku kwa kutoamini kama kweli wametoka salama tena na pointi tatu mbele ya ya vijana wa Kim Poulsen.
Yaya alisema; “Yule aliyevaa jezi namba tano (Kelvin Yondan), ni beki mwenye uwezo mkubwa na nimeambiwa kwamba anacheza soka Tanzania. Kwa uwezo wake anaweza kupambana na mshambuliaji wa aina yoyote hapaswi kuendelea kucheza soka Tanzania.”
“Yule beki alinipa tabu sana kila niliposhika mpira nilifikiri jinsi ya kumpita kwani ana uwezo wa kumkaba mshambuliaji bila ya kusababisha rafu ya aina yoyote, inakulazimu kutumia akili sana kumuingia,”alisema Yaya ambaye amecheza mechi 74 kwenye kikosi cha Ivory Coast.
“Alinifanya nibadili mbinu za uchezaji, nikawa natumia muda mwingi kutoa pasi nyingi kila ninaposhika mpira, labda mimi ningemshauri atafute timu nje ya Tanzania ili apate uzoefu na ataweza kuisaidia timu ya Taifa katika mashindano makubwa kama haya,”alisema mchezaji huyo ambaye aliamua kutumia jezi namba 42 Manchester City baada ya kukuta Patrick Viera akitumia jezi namba 24.
Gervinho ambaye ni straika wa Arsenal aliyeichezea nchi yake mechi 45 akifunga mabao 13 alisema: “Kama tusingekuwa makini na kutumia uzoefu wetu wote Tanzania wangetufunga kwa sababu baada ya yule mchezaji aliyevaa jezi namba 10 (Thomas Ulimwengu) kufunga bao la pili tulichanganyikiwa na kuamini kwamba tusipotumia uzoefu na juhudi binafsi hatuwezi kushinda mechi,”alisema.
“Binafsi nilifarijika sana kucheza na timu yenye wachezaji wenye vipaji vikubwa vya soka, cha msingi wachezaji wajitahidi kutafuta timu nje ya Tanzania hasa katika nchi zilizopiga hatua katika soka, nimesikia mchezaji namba 11 na 10 wanacheza TP Mazembe ni mwanzo mzuri sana lakini wasiishie hapo, pia wengine waige mfano wao na kutafuta timu nje, ingawa kupata timu si kazi rahisi lakini juhudi za mchezaji binafsi zinapaswa kuonekana anapopata timu ya kuchezea.”
Straika aliyepigwa chini na Chelsea na kutimkia Lille ya Ufaransa Julai mwaka jana,  Solomon Kalou alisema; “Mchezaji aliyevaa jezi 10 (Mbwana Samata) anajua. Kwanza anaweza kukaa na mpira, mshambuliaji anayekaa na mpira huwezi kumkaba kwa sababu anajua ni wapi apite ama ni wapi atoe pasi na ili umzuie ni lazima uwe makini kutazama  atakapopeleka pasi yake vinginevyo anakuwa na madhara makubwa,”alisema Kalou.
Akitaja namba za wachezaji wa Stars waliokuwa tishio katika mechi hiyo alisema kwamba ni pamoja na mchezaji anayevaa jezi namba 2 (Sure Boy),10 (Samata), 11(Ulimwengu) na 20 (Shomari Kapombe).
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad