JINI KABULA: NAUMWA, NAHISI N’TAKUFA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

STAA wa filamu na muziki Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amekiri kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukabwa na mashetani usiku na kumsababishia maumivu makali ya mwili hadi kuhisi kufa.

Hivi karibuni Jini Kabula alipotea kwenye ulimwengu wa mastaa jijini Dar hivyo Ijumaa Wikienda likaamua kumtafuta, alipopatikana ndipo likabaini hali yake ni tete kiafya.
Akizungumza na mwanahabari wetu wikiendi iliyopita, Jini Kabula alisema kwa muda mrefu sasa amekuwa mtu wa kuumwaumwa na mwili kukosa nguvu ambapo alishapima vipimo vyote lakini aligundulika kuwa na malaria, akatumia dozi na kuimaliza lakini hali bado siyo nzuri.
Huku akiwa amedhoofu mwili, Jini Kabula alisema kila ikifika usiku wa manane akiwa amelala huwa anakabwa na mtu ambaye hamuoni, hali inayomfanya ashindwe kupumua huku mwili ukikosa nguvu na kuuma kupindukia.

“Nahisi kabisa nakufa kwa jinsi ninavyojisikia mwilini, natamani hata usiku usiingie kwa sababu mateso ninayopata ya kukabwa ni makubwa, wakati mwingine nakesha nikiangalia muvi kwa kuhofia nikilala tu lazima nikabwe.
“Hata rafiki zangu nimeshawaaga na kuwaambia kuwa muda wowote wakisikia nimekufa wasishangae kwa sababu naumwa ila ninayemhurumia ni mwanangu, jamani nitamuacha bado mdogo maskini wa Mungu sijui ni shetani gani ametukumba wasanii,” alisema Jini Kabula kwa masikitiko.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jaribu kile kipimo kingne manake mh!si ulipita kwa mr nice?

    ReplyDelete
  2. pole ila jaribu kupima kile kipimo maana ulipopita mashaka sana mr nice nae si cheche.pima uishi kwa matumaini mpz..pole sana mamii

    ReplyDelete
  3. Anza kunwya dawa wangu. Usikatae kunywa dawa kama wenzio utakufa mapema. Wai wai wai usimfwati daina mamake.

    ReplyDelete
  4. kwani mr nice anao??

    ReplyDelete
  5. Mmmh. Mapepo ya ngono. Kaombewe. Na ngoma pia nice kashakuambukiza

    ReplyDelete

Top Post Ad