Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz Watisha Kili Awards Wajizolea Tuzo za Kumwaga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwaka huu umekuwa mwaka mzuri zaidi kimuziki kwa msanii toka rock City Mwanza Kala Jeremiaha ambae maombi yake kwa ‘Dear God’ yamesikika na amepata majibu kwa njia ya kipekee na wimbo wake ‘Dear God’ umeweza kuchukua tuzo tatu katika Kilimanjaro Music Awards 2013. 

Kala Jeremiah ametumia mkuki mmoja kunasa ‘swala’ wake watatu muhimu mwaka huu, Dear God imeweza kumpa nafasi kubwa na kushinda tuzo katika kipengele cha wimbo bora wa Hip Hop.

Nguvu ya wimbo huo hapana shaka ndiyo imemuwezesha pia kuondoka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop na Mtunzi bora wa mashairi ya Hip Hop.

Kala aliweza kuwapenya wasanii wazito kama Fid Q, Joh Makini, Mwana FA, Profesa Jay na mdogo wake katika game Stamina wa Moro Town waliokutana nae katika vipengele vya Hip Hop.

Wimbo huu ulitengenezwa na mtayarishaji chipukizi Dee Classic ambae pia alikuwa anawania tuzo katika kipengele cha mtayarishaji chipukizi wa Mwaka lakini hakuweza kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kwa Mesen Selector.

Msanii mwingine wa bongo fleva aliyeng’ara katika tuzo hizo ni Ommy Dimpoz ambae pia aliondoka na Tuzo tatu, ambazo ni Video bora ya wimbo bora ya mwaka, wimbo bora wa Bongo Pop ‘Me and You’ akiwa na Vannessa Mdee ambao pia uliwapa tuzo ya wimbo bora wa kushirikishwa/kushirikiana.

Wasanii na watayarishaji wa muziki wa bongo fleva ambao kwa mara ya kwanza wameweza kujishindia tuzo za Kili ni pamoja na kundi la Jambo Squared toka Arusha (Kundi bora la muziki wa kizazi kipya), Rama Dee ‘Kinega’ (Wimbo bora wa RnB ‘Kuwa na subira).

Wengine ni Amini (Wimbo bora wa Zouk Rhumba ‘Ni wewe’), Recho (Msanii bora wa kike Bongo fleva), na Nay wa Mitego (Wimbo bora wa Hip Hop ‘Nasema Nao’). Mesen Selecter (Mtayarishaji chipukizi wa Mwaka), Ali Nipishe (Msanii bora anaechipukia).

Tuzo hizo zimeshuhudiwa huku mfalme na malkia wa muziki wa kibongo wakitangazwa kuwa Lady Jay Dee ‘Anaconda’ (Msanii bora wa Kike) na Diamond Platinumz (Msanii bora wa kiume).
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmmmmhhhhh am verry happy 4dear god tunaomba mwakani apate tunzo nying nyingine big up ommy dimpoz

    ReplyDelete
  2. Ni sawa lakini msanii bora Wa kike sikubaliani mwaka 2012 jaydee hakutoa wimbo wowote ule tuache kuwapa watu tuzo kwa kuangalia historia

    ReplyDelete
  3. Me&u ndo video bora ya mwaka au ni mimi tu sijaelewa, kama ndiyo basi hao majaji walizitandika kwanza hizo kilimanjaro ndo wakaanza kazi, acheni wizi nyie, video gani imechuja vile!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. We nawe hujaelewa,video bora ni baadae,siyo me n you,by the way,u made it Kala,keep it up,next yr ung'ae tena!

    ReplyDelete

Top Post Ad