KAULI YA SEREKALI YA KUTOA MILION MIA MOJA KWA ATAKAYEFICHUA WALIPUA MABOMU HII HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zifuatazo ni nukuu za maneno yaliyotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, sera, uratibu na bunge William Lukuvi kuhusu hilo bomu ambalo lililipuliwa kwenye mkutano cha Chadema Arusha.

“Mtu asiejulikana alirusha kitu katika kundi la watu kilichosababisha mlipuko mkubwa, mkutano huu ulikua na ulinzi wa jeshi la Polisi wakiwa na magari mawili… askari walisimama upande wa Kaskazini ya uwanja ambapo mrushaji alikua mashariki na alirusha bomu kuelekea Magharibi”
“Jaribio la Askari Polisi kutaka kumfata alierusha lilizuiwa na makundi ya Wananchi ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na kuwazomea na hivyo Polisi kulazimika kuanza kujiokoa badala ya kumsaka Muhalifu”
“Mlipuko huo ulisababisha watu wawili kufariki dunia ambao ni Judith William (48) na mtoto Ramadhan Juma (15) na watu 70 wamejeruhiwa miongoni mwao watatu wamejeruhiwa vibaya na wawili hali zao ni mbaya”
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mlipuko huo ulikuwa ni wa bomu la kurusha kwa mkono ambapo pia aina ya urushaji wa bomu hilo haitofautiani na mbinu iliyotumika kwenye shambulio jingine la bomu lililotokea kwenye kanisa la Olasiti Arusha”
“Kutokana na mfululizo wa matukio haya mageni, Serikali imeamua kutenga shilingi milioni 100 kama zawadi kwa mtu yeyote atakaeshirikiana na kutoa taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa muhalifu wa  matukio ya aina hii na mtandao wake mzima” SIKILIZA HAPA:
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad