KWA WEMA WOOTE NILIOMFANYIA HUYU HOUSE GIRL, HII NDIO SHUKRANI YAKE ALIYONIPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ilikuwa miaka kadhaa iliyopita nilipoletewa msichana wa kazi maarufu kama house girl..ukimuangalia kwa sura alionekana mpole na mnyenyekevu.umri wake haukua mdog sana kwani alikuwa na miaka km 20 ivi wkt huo alipofika...alipokuja alionekana wazi kuwa ametoka kwenye familia duni sana kwani hata nguo aliyoivaa ilikuwa imechoka sana..

Nilimpokea vizuri nikamfundisha kazi za nyumbani, na kumuelekeza matumizi ya vitu mbali mbali vya nyumbani kwani hakujua hata jiko la gas linawashwa vipi..Nilimfundisha mapishi mbali mbali ambayo alikuwa hajui kupika..

Alikuja akiwa na begi dogo la marlboro lililokuwa na nguo chache za kuvaa, nilimpa nguo zangu nyingi ambazo zilinibana kwani baada ya mimi kujifungua mwili wangu uliongezeka mara dufu...nikamfundisha usafi wa kuoga asubuhi na jioni ili awe smart na aweze kukaa na watoto akiwa msafi...

alikuwa msikivu na hakuwa mjeuri, niliishi naye kama ndugu yangu na hakika ungenikuta nae tunavyopiga stori usingedhani km ni house girl...kuna watu walijua yule ni ndugu yang kwa jinsi tulivyokuwa tunapatana....nikiwaambia ni house girl hawaamini..

Tuliishi kwa vizuri na hatukuwahi kugombana hata siku moja kwani kwa kiasi kikubwa alitimiza majukumu yake niliyompangia...

Baada ya muda nikaona nimsaidie zaidi kwani pamoja na kuwa ni house girl wang lkn pia alikuwa yatima kwani wazazi wake wote walishafariki dunia..Na pia mtt wangu wa mwisho kwa wakati huo alianza shule kwa hivyo angepata fursa ya kujiendeleza kwani hakukuwa na mtt mdogo aliyebaki nyumbani..

Nikamtafutia shule ya QT ili asome masomo ya sekondari ambayo nilimgharamikia kila kitu..akaanza kusoma hiyo shule kwa makubaliano kwamba atafanya kazi zake zote asubuhi na mchana aende shule..

Nilipokuwa nasafiri na watoto wakati wa likizo au kwenda mapumziko mikoa mbali mbali au nje ya nchi naye pia nilimchukua tukawa pamoja naye..(kumbuka kuwa hapo nyumbani kwangu nilikuwa naishi na watu wengine ambao ni ndugu zangu lkn niliwaacha wao nikawa namchukua yy)

Kila nilipokuwa nasafiri kikazi nilikuwa nawaletea watoto wangu zawadi na yeye pia namletea..

Wakati wa sikukuu nilikuwa nawanunulia watoto wangu nguo mpya na yeye pia namnunulia..na ili kumfanya ainjoi sikukuu yake zaidi nilikuwa nampa pesa ambayo simkati kwenye mshahara wake..

Kila j2 alikuwa free kuanzia saa 4 asb hadi saa 12 jioni, nilimruhusu aende popote lkn ikifika saa 12 awe kesharudi..

Kila mwisho wa mwaka nilimpatia nauli na zawadi za kuwapelekea ndugu zake na wadogo zake na alienda likizo

Nilimkatia bima ya afya na yeye akawa anatibiwa aga khan hospital kama watoto wangu

Nilimnunulia simu ya mkononi na kila simu yake ilipoharibika nilimnunulia nyingine

Kabla sijanunua machine ya kufulia aliniambia yeye hawezi kufua nguo na mikono kwani mikono yake inaharibika na kupata fangas nikamtafuta mtu wa kufua nguo ambaye nilikuwa namlipa..

Kila alipofanya kazi ya ziada kwa mfano kuhudumia wageni au siku za sikukuu ambapo kazi ni nyingi nilikuwa namlipa pesa muda huo huo baada ya kumaliza hizo kazi, na mshahara wake mwisho wa mwezi uko pale pale..

Siku moja moja za wk end nilikuwa namsuka kwani kwa bahati nzuri mie najua kusuka mitindo mingi tu...

siku kama sijamsuka basi nampa hela ya saluni/msusi

siku nikienda naye sokoni/supermaket basi hanunui chochote kwa pesa yake, akitaka kitu namnunulia

kila mwaka unapoisha na mwaka mpya kuingia nilikuwa namuongeza mshahara ili naye ajisikie mwenye thamani.

Kwa muda niliokaa naye aliweza kusave na kununua plot baada ya mimi kumshawishi afanye hivyo ili iweze kumsaidia baadae, japo mimi nilimuongezea pesa kdg iliyopelea.

Nilimuahidi kumsomesha hadi chuo kama yeye angependa na kujitahidi katika masomo ili naye awe na maisha yake baadae..
kichwani mwangu nilipanga kumfundisha gari kwani nilishamchukulia km ndugu yangu...hili nilikuwa sijamwambia, nilitaka amalize kwanza elimu ya sekondari.

NOTE
kwa nature ya kazi yangu huwa nasafiri mara kwa mara lkn nikiwa nyumbani lkn huwa sina tabia ya kujibweteka na kumuachia house girl afanye kila kitu...
Kila siku jioni napika chakula cha usiku baada ya kurudi kazini, nikichelewa namwambia apike cha watt na watu wengine, changu na cha baba napika mwenyewe nikifika...mara nyingi mimi na mr tunakula ugali wao wanapenda wali, n.k

nafanya usafi wa chumba changu choote hadi washroom mara 3 au 4 kwa wiki

nafua nguo zangu na za mume wng zote siku ya jumamosi.

siku ya jumamosi na jumapili naingia jikoni kuanzia asb hadi jioni, except kama nimeenda kazn au nimepata dharura..siku za wk end asb huwa natengeneza mchemsho kwa ajili ya familia....na pia napika mwenyewe chakula cha mchana na usiku..(binafsi huwa sipendi kupikiwa hasa nikiwa nyumbani kwani nahisi km chakula kina kasoro nyingi km atapika m2 mwingine,) kwa ivo huwa naingia jikoni mwenyewe.


ALICHONIFANYIA SASA
Baada ya miaka kadhaa nikahisi kama anabdilika na kuwa jeuri lkn sikujali saana, nilijua tu labda yuko days hivi ambayo wkt mwingine yanasababisha mood kuchange..

Nilikuwa na mpaka leo huwa simruhusu house girl kuingia chumbani kwang kwani usafi na kila kitu huwa nafanya mwenyewe hata kama nina mimba ya kujifungua leo..
Sasa kuna kipindi niliposafiri nilikuta kitanda changu kimetandikwa vizuri mpk nikawa na was was, sbb mume wangu huwa hatandiki wala habadilishi shuka mpaka nirudi safari...Siku moja nilimuuliza mume wng nani kamtandikia kitanda? kwani najua kbs hata km ni yeye katandika hawezi kunyoosha shuka vizuri, mara nyingi mume wng yupo rafu, akaniambia amemuomba house girl amsaidie kutandika, nikamuuliza tangu lini house girl anaingia chumbani kwng? akasema samahani mke wng sitarudia tena...nikanyamaza moyoni nikaanza kuwa na shaka lkn sikufatilia saana... huyo house girl siku zooooote hakuwahi kuingia chumbani na mimi sijawahi mruhusu, iweje kipindi hicho tena nikiwa nimesafiri aingie? hapo alikuwa kashakaa muda wa kutosha na keshakuwa mzoefu ila sio chumbani kwang...ila nikapotezea kwani baada ya hapo ikawa hata nikisafiri nakuta vile vile chumba kipo rafu rafu, hakujatandikwa kama zamani, nikajua ni kweli ilikuwa msaada tu kwa mr na nikafutilia mbali was was wng...

Miezi miwili baadae huyo house girl akaniaga gafla akisema bibi yake ni mgonjwa anaumwa, kwa sbb nilikuwa na namba za simu za ndugu zake nikawauliza wakasema kweli bibi yake anaumwa, nikamruhusu aende kumsalimia..akaondoka, lkn kilichonishangaza ni pale alipokusanya mabegi ya nguo zake zote, viatu vyake vyote n.k nikamuuliza mbona umekusanya kila kitu hutegemei kurudi? akasema anaenda kuwagawia ndugu zake yeye ataanza upya akirudi..na vile alikuwa bado anasoma sikumtilia shaka nikajua atarudi tu...

alipofika kwao tu akanitumia ujumbe mfupi wa simu akisema yeye hatarudi tena na ameamua kusomea huko huko kwao.....aaaaaaaaaahhhhhhhhhhh nilikuwa so much dissapointed sbb wakati huo mi nilikuwa mjamzito tena nakaribia kujifungua...kuna ndugu yng alinionea huruma akaniletea msichana wake anisaidie...

Baada ya muda nikasikia yule house girl wang aliyeondoka ni mjamzito, sikufatilia ila nikajua ndio sbb iliyomfanya aondoke nyumbani kwng..

Baadae akajifungua nikaambiwa, nami nikampigia simu kumpongeza, na pia nikamnunulia zawadi za mtt nikampa mtu ampelekee...lkn pia mara kwa mara nilikuwa nampigia cm na kumsalimia yy na mwanae..

MIAKA KADHAA BAADAE ndio nikaja kujua kuwa huyo mtt wa house girl wangu ni wa mume wangu...
Nilipomuuliza mume wng alikubali na kuniomba msamaha saaaana, akasema huyo house girl kila nilipokuwa nasafiri alikuwa akivaa kanga moja na kujilengesha sana mpk akaingia kwny mtego.

SIWEZI SEMA, MAUMIVU niliyopata hayaelezeki.....
NI MIAKA KADHAA imepita toka tukio hili kutokea, lkn mpaka sasa bado nasikia maumivu yake moyoni....in fact ht jana uck nilikosa usingizi baada ya kukumbuka tukio hili, nikajikuta machozi yananitoka bila kuyazuia...

kwa wema wooooote niliomfanyia huyu house girl kweli hii ndio shukurani yake?,yaaani sina hamu..na mpk leo hii sina hamu...nilibaki nimeshikwa na butwaa..
japo hiyo haijanifanya niwachukie mahouse girl wengine lkn sina hamu nao kabisa hawa watu...
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

28 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ukome kusafiri safiri na kumuacha mmeo. We ulitaka amfanye nani sasa. Mxiiii

    ReplyDelete
  2. Mume hulindwa kwa MAOMBI.Not by cooking nice food or prohibiting ua housegirl asiingie chumbani kwako nk.Maandiko yanasema mke atamlinda mume wake.Pole,samehe and stop lebeling events that ar good or bad.,Just knw that the world is a giant rader,ht teaches u everyday when u go out.

    ReplyDelete
  3. pole limeshatokea na mume wako alikwambia ukweli na kukuomba msamaha sasa unalia nn sahau na kusamehe

    ReplyDelete
  4. pole limeshatokea na mume wako alikwambia ukweli na kukuomba msamaha sasa unalia nn sahau na kusamehe

    ReplyDelete
  5. Pole sana Dada kwa yaliyo kukuta Mara nyingi sana house girl anapo pendeza na mama mwenye nyumba anapokua nje ya nyuma kwa siku Kadhaa hapo lazima Mwanaume atageuza kibao tu Kwa House Girl yaani ili kuilinda ndoa yako lazima upunguze safari za nje ya nyumba kwa zaidi ya siku 3.hata yeye angekua anasafiri na nyumbani unabaki na house boy na kila siku Kabla ajaondoka mlikua na kawaida ya kila siku USIKU Kuvinjali hapo lazima itakula kwake,Makosa sio ya house girl hapo makosa ni ya Mumeo maana ndio yeye aliye mshawishi uyo house girl.Wavunje amli ya 6 ya Mungu

    ReplyDelete
  6. Usichukie housgerl wanaume wote wanafanana afadhari mumeo anakuomba radhi Wa kwangu kila housegirl anatongoza na huko nje ndio usiseme ukimuuliza wal hajali, msamehe mumeo Kama huwezi chukua taraka yako, lakini wanaume wote ndivyo walivyo labda awe hanithi Naye atakuwa shoga

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe acha hizo unachosema sio sahihi hata kidogo, wanaume wote hawako hivyo labda huyo mumeo ndio yuko hivyo mbona mimi sijawahi tembea na house girl. Mke wangu ananiridhisha kama wewe humridhishi mumeo shauri wacha beki 3 amburudishe

      Delete
  7. Sasa jamani...kwa kuandika hii story hapa..unataka kuwafundisha watu wengine.. some sort of a lesson au ni ili ikusaidieje wewe??
    Kama unaona its too much fanya counseling with specialists but..wow haya ni mambo ya ndani kati yako wewe na mumeo...
    Deal with it like a mature lady...through proper channels...

    ReplyDelete
    Replies
    1. bora umwambie sioni sababu ya mada yake, kwanza ni uongo mtupu

      Delete
  8. Yaani wewe unasafiri nyumbani unamuacha paka na panya unategemea nini? Hata ingekuwa mimi ningekula tu. Lakini hata wewe kule ulikokuwa unaenda si ulikuwa unaliwa?

    ReplyDelete
  9. pole sana mamii,lak usimlaumu house girl mlaumu mumeo maana yule binti ni mdogo na mumeo ni mtu mzima I hope so,inawezekana anakudanganya kusema kwamba binti alikua anamvalia kanga moja!!inawezekana yeye ndo kamlazimisha huyo binti!! ukweli wanaujua wao. KIKUBWA NI JITAHIDI SANA KUMLINDA MUMEO KWA MAOMBI MAANA WANAUME WAKO WEAK SANA KWA WANANAWAKE HAWAJALI NA HATA ANGEKUA MDOGO WAKO ANGEMDO,CHA MSINGI KAMA MUMEO AMEKUOMBA MSAMAHA NI WEWE KUMSAMEHE,NA WEWE UNASAFARI SANA,HAKIKISHA UNAPOSAFIRI MUACHE MUMEO KATIKA HALI NZURI,NAMAANISHA KIMAPENZI!! ILI ANGALAU HATA UKIKAA SIKU 3 HATOKUWA NA TAMAA YA HARAKA SANA.INCASE KAMA UMESHAPATA MSICHANA MWINGINE KWA USHAURI WANGU KAMA UNASAFIRI HAMISHA WATOTO NA MSICHANA WA KAZI WAPELEKE KWA MAMA YAKO AU NDUGU YAKO YOYOTE AMBAPO UNAAMINI WATAKUA NA AMANI YA KUISHI HAPO,MAANA MUMEO ANAONYESHA YUKO WEAK SASA ASIJE AKAFANYA NA KWA HUYO MWINGINE NA NDIO ITAKUUMIZA ZAIDI.

    ReplyDelete
  10. haya someni fanyeni kazi nzuri...pateni mi hela ndoa unaisahau kazi kupiga picha za instagram ukiwa na mashoga zako wasomi wenzio mara mkanunue brazilian..sio kosa lako usijilaumu..kwanza wanaume wote malaya..ushauri wangu live ur life..msamee kama utamsamehe mpotezee kama utataka.tenda wema nenda zako

    ReplyDelete
  11. Pole sana dada lakini amini kila mtu anammitihani yake tofauti katika maisha matatizo hayafanani wewe unaumizwa na hiki mwingine na kile jitahidi kuyashinda

    ReplyDelete
  12. wewe Joseph Malisa hayajakukuta ndo maana unasema ya kutunga hiyo ngoja hata nduguyo wa karibu yatamkuta then useme ya kutunga na sio woote wana roho za kulipiza

    ReplyDelete
  13. dada usimchukia maid wako ila wanaume ndo walivyo cha muhimu omba kama huyo maid alikuwa hana kidumu kingine magonjwa mengipia kumbuka shukrani ya punda ni mateke

    ReplyDelete
  14. duh tatizo wanawake ukishaolewa na kuzaa kwenu mmefika
    wanaume huwa twahitaji mitego na manjonjo co kunenepeana tu!!mtaendelea kusaidiwa mpk mwisho wa dunia

    ReplyDelete
  15. Hope sister is here for our help and advice. If u hv no any of these better read and disapear than dispising or inplanting ur own feelings abt men and ladies. For u who say and do that it is evident that u are referring to ur own past experiences.Please stop it and mean postives wat this network is here4.Lady if ur guy's sory is real accept it and make necessary corrections on ur side if any.Play that God helps u 4get all these misfortunes and change ur man for better forever.Arrange self and together players wirh him.Hope that way gonna win back his max love and he will always be there for u and family.May God bless and guide u through out.

    ReplyDelete
  16. Mtu kumwacha Mume au Mke siku kadha bila kuheshimu ndoa ni hatari sana, kumbuka mwili wa mwanadamu ktk maswala ya mapenzi huwa unaamka pale unapoona kitu kinacho husiana na ngono kama vl movie picture ama mwanamke au mwanaume anapoonyesha sehemu za ndani ya mwili ama kwa bahati mbaya au makusudi. Worning... Kwa walioowana huwa miili yao imezoea mapenzi na inapotokea mmoja kuwa mbali kwa muda mrefu, hii hufanya usiku kuwa mrefu na wa mawazo meng yakiambatana na hisia za kitandani. Ss inapotokea mara nyng, uvumilivu huwa mgumu mara kwa mara na hasa ukizingatia hisia za mapenz kuna wakat huwa juu sn. Inapotokea house boy au girl anakuwa karibu na ktk mazingira ya kwao peke yao, yaani hakuna watu wengi ktk eneo hilo, uharibifu ni lazima hasa kw wa2 wasio na hofu ya Mungu. Maandiko yanasema, ikimbieni zinaa. Utawezaje kukimbia ikiwa wakati wote iko malangoni mwako? Cc n wanadam na hata kwako yaweza kukutoke na hata ukawa unashangaa menyw imekuwaje mpaka kufanya hivyo? Mwanadamu wasil hupenda mambo ya mwilini. Unaposamehe, inakupasa kusahau na c kukumbk. Mungu anasema, usipo samehe hutosamehewa na ndo maana MUNGU anasema, nitakusamehe na kuyasahau maovu yote. Na c kusema nimekusamehe lakn sitasahau. Jaman, nimepta njia isiyo yangu ila ukimkuta mwnye shida utamsaidia japo c njia yako. Nina meng sn ila, maisha ya ndoa yanahitaji sn Mungu wa mbingu na ni safari ndefu isiyo na formuler.. Wajuzi ni nyie, kucheka na kulia ni kawaida na ndo maana kuna kupanda na kuvuna. Ndoa na iheshimiwe na watu wote.

    ReplyDelete
  17. pole sana dada maisha ya ndoa ndio yalivyo, uvumilivu unahitajika ile mbaya

    ReplyDelete
  18. Uongo mtupu huo, hakuna mke anamfanyia housegirl hivyo vyote, stori ya kutunga hii, dunia ya sasa hakuna anayefanya yote hayo kwa housegirl.

    ReplyDelete
  19. Wapo watu wanaofanyia ma-housegirl wema. Kuna nyumba ukienda huwezi kutofautisha housegirl na watoto wa nyumbani. Huyu dada alishaona housegirl ni yatima akaamua kumsaidia. Mi nina housegirl anayekaa kwamgu na mtoto wake. Ni yatima na mwanaume aliyezaa nae kaingia mitini. Sitakaa nae maisha yote. Nasubiri mtoto wake akue aweze kwenda chekechea ili mama yake akajifunze ufundi anaouweza nimpe kiinua mgongo waondoke kwangu. Akizini na mume wangu wala sitauliza kama alibakwa au la. Kama alibakwa mbona hakusema? Namtimua kama sina akili nzurindo nirudi chumbani kupambana na rijali wangu. Ila nilichojifunza binadamu wengi hasa wasio na hofu ya mungu wakipewa favour muda mrefu huwa wanajisahau na kuanza kuzihesabu kama haki na kuanza kuleta kiburi na badala ya shukrani.

    ReplyDelete
  20. Pole sana kwa yaliyokukuta, wakati wa uumbaji wanaume tuliumbiwa 'tamaa' tukapewa utii, na wanawake mliumbiwa 'upendo' mkanyimwa utii na ndiyo maana kwenye vitabu vitakatifu mnaaswa siku zote kuwa "enyi wanawake watiini waume zenu, na wanaume wapendeni wake zenu"
    Kwa hiyo sisi wanaume hutamani kila kitu kilicho mbele yetu ilimradi kina jinsia tofauti ya kwetu, tunakumbana na vikwazo vya kwamba huyu ni mtoto wangu, dada yangu, mama au mama mdogo, ukiacha uhusiano wa karibu mwanaume hutamani kila mwanamke aliyembele yake. kwa sababu ya tamaa ya mumeo lazima ndiye aliyechochea kuzini na housegirl na si kweli kuwa housegirl alikuwa akimvalia kanga moja.Nini kanga moja hata angekaa mbele yake mtupu kama alivyozaliwa kama ni mwanamume mwenye kumuogopa mungu na kuheshimu uwepo wa mungu basi angemkemea na wala asingelazimishwa kuzini nae. katika maisha yangu sijawahi kusikia mwanamke amembaka mwanamume, kwa hiyo tamaa ya mumeo na kutokuiheshimu ndoa yenu ndiko kulikomsukuma kudate na housegirl wenu.
    Na huenda mumeo ndiye aliyetoa wazo la kumtafutia shule na huenda siku za jumapili mumeo pia alikuwa anakwenda kokote kuanzia saa 4 hadi saa 12 kama ulivyokuwa ukimpa nafasi ya kutoka na kwenda atakako.
    Mwanamme kama anamsimamo hayumbishwi na kanga moja, mlaumu mumeo housegirl yatima aliyetoka kwenye familia duni kupata bahati ya kutembea na mumeo yeye kwake ni bonge ya promotion na hakuna housegirl anaeweza kukataa. Tena mshukuru sana mumeo la sivyo siku moja ungeambiwa mama fungasha nenda zako housegirl akatwaa madaraka, wanawake wengi wamelizwa sana.
    Pole sana na wala usikose usingizi wanaume tumeumbiwa tamaa, kwani hujawahi muona mumeo uko nae kwenye gari anaendesha na akikatiza mwanamke anageuka kumtazama wakati wewe upo ubavuni mwake?

    ReplyDelete
  21. pole sana kwa yaliyokukuta kama mumeo alikuomba msamaha na umekubali kumsamehe ni vizuri. Na hawa mabeki tatu wengine wanavisa balaa wanajua kabisa kanga moko inawafanya wawavutie wanaume wakati mwingine mitego mingine haikwepeki

    ReplyDelete
  22. This lyf bwana..!

    ReplyDelete
  23. Hivi hyo pcha hapo juu ndo mfanyakaz au?

    ReplyDelete

Top Post Ad