Lwakatare"Nitafunguka na Kutoa ya Moyoni Alhamisi"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare amesema atatoa ya moyoni siku ya Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi mara baada ya kupata dhamana aliomba subira kwa watanzania kwani anayo siri nzito moyoni.

Lwakatare alisema anawaomba waandishi wa habari watulie kwani anatarajiwa kuzungumza kwanza na viongozi wake wakuu wa chama na jopo la wanasheria wake nguli ndipo azungumze na dunia.

Wakati hayo yakiendelea mtandao wa You Tube unamuonyesha Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akitamba kwenye kampeni za udiwani Arusha kwamba ndiye aliyegharamia vifaa vyote vilivyotumika kumrekodi Lwakatare na hatimaye mateso yote yaliyomfika Lwakatare.

Viongozi wakuu wa Chadema tayari wameelezea furaha yao baada ya Lwakatare kupata dhamana.Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe yuko Dodoma katika vikao vya bunge wakati Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa yuko kwenye ziara ya kichama barani Ulaya.Katika salamu zake jana alizozitoa akiwa Ujerumani Dr Slaa alimpa pole Lwakatare na hapo hapo kuelezea furaha yake na ya watanzania wanaoishi Ujerumani kwa Lwakatare kupata dhamana na kuweza kuungana na familia yake tena baada ya mateso ya miezi mitatu.

Source:Tanzania Daima.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad