google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html MAMA KANUMBA, MAMA LULU WAGEUKA KITUKO KWA UJIO WA KANUMBA MPYA | UDAKU SPECIAL

MAMA KANUMBA, MAMA LULU WAGEUKA KITUKO KWA UJIO WA KANUMBA MPYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila wamegeuka kituko baada ya kunaswa wakishangilia kumpata ‘Kanumba mpya’.

Tukio hilo ambalo liliwafanya watu wengi wapigwe na butwaa, lilitokea  hivi karibuni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wamama hao ambao watu hawakudhania kama ni mashosti, walisikika wakipiga shangwe wakisema wamepata mtoto wa kiume kupitia kwa mtoto wa mama Kanumba aitwaye Adela kisha kumfananisha na marehemu Kanumba.
Mwandishi wetu ambaye alikuwepo eneo hilo, alipowauliza kulikoni wapige kelele nyingi za shangwe, mama Kanumba ndiye alikuwa wa kwanza kuzungumza:
“Tuna furaha sana kuzaliwa kwa Kanumba The Great leo, tulikuwa tukimsubiri kwa hamu sana na hatimaye leo amezaliwa.”
Wakati mama Kanumba alipokuwa akimalizia kuzungumza, mama Lulu naye akadakia:
“Kipindi chote tulikuwa tukiomba sana tumpate mtoto wa kiume na tulikuwa tumepanga tumpe jina la Kanumba kwa hivyo hapa tuna furaha kumpata Kanumba mpya.”
Mama Kanumba na mama Lulu kwa sasa wanadaiwa kuwa ni marafiki wa kutupwa na mara nyingi wamekuwa wakinaswa katika viwanja tofauti vya starehe jijini.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad