MWANAMKE AIBA NYAMA HOTELINI NA KUIFICHA SEHEMU ZA SIRI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WENYEJI wa eneo la Kibung’a, Kaunti ya Tharaka Nithi walijionea sinema ya bure, mwanamke mmoja wa umri wa makamo alipopatikana ameiba kipande cha nyama na kukificha katika sehemu zake za siri.

Kulingana na wenyeji hao, mwanamke huyo aliingia katika hoteli moja ambapo nyama hupikwa na kuuzwa na kuagiza kikombe cha supu.
Baada ya kuinywa supu hiyo, mwanamke huyo alimpatia muuzaji pesa lakini muuzaji huyo akawa hana pesa za kumpa salio lake. Ilimbidi muuzaji huyo atoke nje akatafute 'chenji’ na kumwacha mwanamke huyo hotelini peke yake.

Punde tu alipomwona muuzaji ametoka nje, mwanamke huyo alinyemelea mahali ambapo kulikuwa na nyama, akakichukua kipande kimoja na kukificha kwa 'baika’.

Akiyafanya haya yote, mwanamke huyo hakuwa na habari kwamba alikuwa akichunguliwa na wanawake ambao walikuwa wakiuza ndizi karibu na hoteli hiyo na ambao walimuarifu mwenyewe punde tu aliporejea.

Kizaazaa kilichozuka kiliwavutiwa watu wengi ambao walikuwa sokoni huku kila mtu akitaka  kumpiga mwanamke huyo.

Polisi

Kwa bahati nzuri polisi kutoka kituo cha polisi cha Kibung’a walipashwa habari kuhusiana na kisa hicho na kufika mahali hapo kwa kasi. Mwanamke huyo aliokolewa kutoka kwa hasira za wenyeji.

Walimzuilia katika kituo cha polisi akingoja kufikishwa mahakamani ambako atashtakiwa kwa kosa la wizi.

Duru zinaarifu kuwa mwanamke huyo alianza kuiba baada ya kukatazwa kupika pombe haramu kufuatia msako mkali unaoendelea katika eneo hilo unaolenga kusitisha utengenezaji wa pombe haramu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad