Naibu Spika Ndungai Apinga Vikali Spika Kutokuwa Mbunge

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amepinga mapendekezo ya rasimu yanayotaka Spika na msaidizi wake wasitokane na vyama.

Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa aliiambia Mwananchi jana kuwa ni kitu kizuri kwa Spika kuwa miongoni mwa wabunge.

“Mimi nadhani kuna tatizo hapa. Pamoja na kwamba ni rasimu, lakini ni kosa kwa Spika kutokuwa na chama.

“Hivi kweli, kuna umoja wa madaktari, halafu kiongozi wao atoke nje ya fani ya udaktari, sidhani kama kutakuwa na ufanisi na kuelewana hapo,” aliongeza Ndugai.Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa suala zima ni mapendekezo, na litakuja hadi Bungeni kwa majadiliano na hii itapata changamoto nyingi.

source gazeti la mwanainchi leo.

Maoni yangu, huyu bwana asijifagilie nakumbuka nchi hiihii bunge hilihili la ambalo nae NDUGAI amebahatika kuwa mbunge liliwahi kuwa na spika ambae hakuwa mbunge ambae nakumbuka alikuwa akiitwa Chifu Adam Sapi Mkwawa, bunge aliliendesha vizuri kabisa kwani tatizo lilikuwa nini

Mhe NDUGAI akubali matokeo, spika bila kuwa bunge inawezekana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu ndugai hana akili. Huwezi kufananisha madaktari na wabunge. Udaktari ni taaluma inayomghalimu mtu si chini ya miaka mitano ya kuosomea. Ubunge ni swala la mtu kuwa na umri wa miaka ya kuchaguliwa tu. Hakuta utaalamu wowote wa kuwa spika.. Tunataka mti asiye na chama ili kuwe na usawa na haki bungeni.. Tatizo ccm wanaogopa kupoteza nguvu ya kukandamiza upinzani bungeni.. Kuhusu kama inafaa au haifai spika kutokuwa mbunge tuache sisi wananchi tuamue katika kura za maoni. Sio wewe.

    ReplyDelete

Top Post Ad