P Funk Majani Asukuma Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Mangwear

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWANDAAJI wa ala za muziki nchini Tanzania  P Funk Majani alichanganyikiwa baada ya kuona jeneza iliyokuwa imebeba mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea.
P Funk ambaye muda wote alikuwa amekaa kwenye gari akiwa na huzuni mkubwa kufuatia kifo cha msanii huyo, alibadilika ghafla baada ya kuona jeneza hilo likiingizwa katika gari maalum tayari kwa ajili ya safari kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
P Funk alishindwa kujizuia na akalazimika kushuka kwenye gari lake na kwenda kusukuma gari lililokuwa limebeba mwili wa msanii huyo aliyefariki Dunia Mei 28 mwaka nchini Afrika Kusini.
Kitendo cha P Funk kusuka gari hilo huku akibubujika machozi kwa zaidi ya dakika mbili ilihamasisha mashabiki wa msanii huyo na kuungana naye kusukuma gari hilo.
Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakazi wa jiji la Dar es Salaam kesho watapata fulsa ya kutoa heshma ya mwisho kwenye jeneza la marehemu Mangwea katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mjini Morogoro kwa mazishi kesho kutwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Daaaah so sadnecc situation bt mola kampenda zaid!.

    ReplyDelete
  2. mbele yake nyuma yetu, kazi ya mola haina makosa

    ReplyDelete
  3. dah! Hyo imetuumiza wengi cha msingi tumtangulize mungu kama mfariji wetu kwny hiki kipindi kigumu cha majonzi..R.I.P Albert Mangwea.

    ReplyDelete
  4. Mungu kampenda zaidi R I P Albert Mangwea

    ReplyDelete
  5. r.i.p cowbermer

    ReplyDelete

Top Post Ad