Stars Yatibua Safari ya Brazil

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo ilitia doa safari yake ya kwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Marrakech, mjini hapa.
li kusonga mbele, sasa Taifa Stars italazimika kushinda mechi zake mbili za mwisho, dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Dar es Salaam, kabla ya kusafiri kwenda Gambia.
Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo ilitia doa safari yake ya kwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Marrakech, mjini hapa.
Katika mchezo huo, Stars ilihitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri, lakini ilijikifungwa mabao hayo mawili, moja katika kila kipindi, huku bao la kufutia machozi likifungwa na Amri Kiemba.
Matokeo hayo, yameifikisha Morocco pointi tano, lakini ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, na Stars imebaki na pointi sita nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast iliyoifunga Gambia mabao 3-0 na kufikisha pointi 10.
Kipindi cha kwanza kilishuhudia Taifa Stars ikipelekwa puta na wenyeji wao waliotawala sehemu kubwa ya kiungo na hivyo kuruhusu mashambulizi mengi yaliyomnyima nafasi ya kupumzika kipa na nahodha Juma Kaseja.
Stars ilimtumia mshambuliaji mmoja mbele, Thomas Ulimwengu na kufanya mashambulizi ya kushitukiza langoni mwa wapinzani wao.
Morocco wangeweza kufanya matokeo kuwa tofauti katika dakika za 5, 9 na 13 kama siyo Yousef El Arab, Hermach na Barrada kushindwa kumtungua kipa wa Stars.
Stars uliyokuwa ikishangiliwa na mashabiki 300, walibisha hodi lango la Morocco dakika ya 20 baada ya beki Shomari Kapombe kumjaribu kipa wa Morocco, Nadir Lamyaghri kwa shuti la mbali lililopaa juu ya lango.
Dakika tano baadaye Ulimwengu, alikuwa kwenye wakati mzuri wa kuipatia bao Stars baada ya kupokea mpira mrefu na kukimbia nao mpaka ndani ya boksi la hatari lakini akapiga kiki dhaifu iliyodakwa na Lamyaghri.
Mfumo wa Stars kucheza kwa kujiami zaidi kuliko kushambulia uliendelea kuleta hali ya mashaka langoni mwao, ambapo dakika ya 38 Morocco walipata bao la kuongoza kwa kiki ya penalti.
Penalti hiyo iliyokwamishwa wavuni na Abderazak ilitokana na faulo ya beki wa Stars, Aggrey Morris aliyemwangusha ndani ya dimba la hatari mshambuliaji Issam el Edoua.
Morocco alitumia mwanya wa Stars kucheza pungufu na kufanya, ambapo mwanzoni mwa robo ya kipindi cha pili, waliongeza bao la pili kupitia kwa Yousef aliyepita katikati ya ngome ya Stars na kumpiga chenga Kaseja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ng'ombe wa maskini hazai!

    ReplyDelete
  2. Bado kuna nafasi, inawezekana mambo yakawa yetu hivyo tusikate tamaa, hata maji yenyewe yakitibuliwa baada ya mda utulia na ata yaweza tumika kwa kunywa. Big-up Stars, Big-up wantanzania wote Na zaidi Big-up my Great Land (TANZANIA).

    ReplyDelete

Top Post Ad