STEVE NYERERE: NATESEKA NA UGONJWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu iliyopita nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar, Steve alisema anasumbuliwa na mkono wa kulia ambao umevimba na kutoa maji kiasi cha kumfanya usiku asiweze kupata usingizi mpaka achome sindano.
“Mkono umevimba, unatoa majimaji kama vile nimeungua na moto na mifupa inaniuma sana kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zangu,” alisema.
Staa huyo alimwambia mwandishi wetu kwamba chanzo cha ugonjwa huo ni maralia iliyompata na kwenda hospitali ambako aliandikiwa dawa mseto.
“Nilitumia dozi ya kwanza, kisha ya pili hapo ndipo tatizo lilipoanza, hospitali wanasema nina aleji,” alisema.
Hali hiyo imemfanya Steve kudhoofu na muda mwingi kushinda ndani kwa takribani wiki mbili sasa kwa kuwa mifupa ya mkono huo inamuuma sana hususan usiku unapoingia.
Aidha, Steve amewashukuru mastaa wenzake wanaompa sapoti kwa kumtembelea na kumjulia hali na akawataja wachache kuwa, ni Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’ Mama Rolaa na Sabrina Rupia ‘Cathy’.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad