THAMANI YA KIEMBA NI SH 500MIL

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dar es Salaam. Wakati Simba ikiendelea kusotea pesa za kuuzwa Emmanuel Okwi klabu ya Etoile du Saleh ya Tunisia, klabu hiyo imesema mpango wake wa kumpiga bei kiungo, Amri Kiemba kwenda Raja Casablanca ya Morocco utatimia iwapo klabu hiyo itakubali kutoa siyo chini ya Sh500 milioni.

Raja Casablanca imepiga hodi Msimbazi kutaka kumsajili Kiemba baada ya kuvutiwa naye wakati walipomwona akiichezea Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Morocco zaidi ya wiki moja iliyopita.

Akizungumza na Mwanannchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspope alisema, kiwango hicho cha fedha ndiyo thamani ya sasa ya Kiemba.

“Tayari tumezungumza na Raja Casablanca na kweli wameonyesha nia ya kumtaka Kiemba, lakini kwetu hakuna namna yoyote ya kumtoa bila Sh500 milioni kuwekwa mezani,” alisema Hanspope.

“Nilipokwenda kwao (Morocco) Rais wa klabu alikuwa Uturuki, tunasubiri arejee ili tuwatumie mchanganuo mzima wa mauzo ya Kiemba,” alisema.

Hanspope, alisema angependa kuona klabu yake inafanya biashara ya kuwauza wachezaji kwa faida. Tunatakiwa kuwalipa makocha, kuingia mikataba na wachezaji, mambo yote haya yanahitaji pesa. Hatuwezi tena kufanya biashara isiyo na faida kwa upande wetu,” alisema zaidi bosi huyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Halafu kazi halisi ya wanaojiita wadhamini wa Simba ni ipi?au ni usajili wa mbwembwe 2 na kufukuza makocha?

    ReplyDelete

Top Post Ad