7 Jun 2013

Ulevi, Uzinzi na Starehe Vimemponza Mr.Nice

Ni wiki kadhaa tu zimepita ambapo Nice Lucas Mkenda aka Mr. Nice alirudi kwa kishindo kwenye vyombo vya habari. Baada ya kusaini mkataba mnono na GrandPa Records ya Kenya, Nice aligeuka kama mfalme
Kwa muda mfupi alifanikiwa kufanya interview kwenye radio na TV zote kubwa za Kenya. Nice alitawala headlines za magazeti na hata blogs za burudani kutokana na watu kuamini kuwa huo ni ujio mpya na wa kishindo wa msanii huyo aliyekuwa amepotea kabisa.

GrandPa Records waliita wana habari waliomuuliza maswali kwa shauku Mr. Nice ambaye aliyajibu kwa ufasaha na ustadi mkubwa. Kwenye interview za TV na radio, Nice aliongea kwa mamlaka na kujiamini, kitu kilichotupa ishara kuwa, msanii huyu aliyekuwa na sifa mbaya za ulevi amebadilika kabisa na kwamba hii ndio nafasi yake ya pili kurekebisha makosa yake na kurudi tena kileleni.

Kumbe tulikosea. Nice alikuwa amebadilika kwa nje tu lakini ndani alikuwa ni yule yule. Maisha magumu na kusota mtaani havijambadilisha chochote. Kwa muda mfupi tu tangu achukuliwe na label hiyo, Nice alitoa makucha yake na kugeuka kuwa mzigo.

Inadaiwa kuwa Nice alianza kuwakera GrandaPA kwa tabia yake ya ulevi, kushindwa kwendana na ratiba ya studio na kuonesha picha mbaya kwa label hiyo. Kwa mujibu wa Pulse ya Standard Media, Kenya, Mr Nice aliwahi kupigana na dereva aliyekuwa akimwendesha, Oro kwenye studio. Pia alikuwa na tabia ya kuingiza wanawake na kulewa studio.

CEO wa Grandpa, Refigah aliiambia Pulse kuwa kuna siku Nice alilewa hadi kushindwa kulipa bili hali iliyomlazimu promoter aitwaye Dickson kumuokoa. Aliongeza kuwa nusu ya pesa aliyokuwa akiipata ilikuwa ikiisha kwa kuinywea pombe ama kula bata na wanawake.

Refigah alidai kuwa kuna wakati Nice alikuwa akilewa hadi kuanza kuwachezea na kuwasumbua wanawake studio. Kulikuwa na ratiba afanye collabo na Ragga D na Nameless lakini ilishindikana kutokana na tabia yake mbaya.

Siku moja kabla ya kuitisha waandishi wa habari kutangaza uamuzi wa kumpiga chini, label hiyo ilikuwa busy kumnyang’anya kila kitu walichokuwa wamempa. Walienda kwenye nyumba waliyokuwa wamempatia jijini Nairobi na kuchukua furniture zote walizokuwa wamemwekea mbele ya mashahidi na polisi.

Tunasubiri kusikia upande wa pili wa story hii kutoka kwa Nice mwenyewe lakini kama ndivyo alivyofanya basi amezingua mbayaaaaa!!

Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment


Popular Posts

Matangazo

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger