HIZI NDIZO PICHA ZA UGONI ZA NDIKUMANA NA LUCY KOMBA ZINAZOMTESA IRENE UWOYA.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

LILE sakata la staa wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya kutuhumu kumshika ugoni staa mwenzake aliyemtoa kwenye gemu, Lucy Francis Komba limeingia sura nyingine kuafutia picha za filamu inayodaiwa kuchezwa na wawili hao kunaswa na Ijumaa, twende hatua kwa hatua.

Katika baadhi ya matoleo ya Magazeti ya Global Publishers zilichapishwa habari za mastaa hao kuzua bifu zito kufuatia Lucy kumchukua mwanasoka wa Rwanda ambaye ni mume wa ndoa wa Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ na kucheza naye filamu jambo ambalo Uwoya alilipinga. KWA NINI UWOYA ALIPINGA?
Uwoya alipinga mumewe kushiriki filamu hiyo kwa sababu aliambiwa washiriki ni wawili tu, mumewe Ndikumana na Lucy. Filamu inaitwa Kwa nini Nisimuoe?
Kwa mujibu wa Uwoya, hajawahi kuona filamu ya kawaida inachezwa na watu wawili tu, akasema Lucy alitumia nafasi hiyo kuwa na mumewe kimapenzi.
Hata hivyo, Uwoya alisema akiviona vipande vya picha za filamu hiyo atajua ukweli.
Wiki iliyopita aliviona vipande hivyo na kuweka msimamo wake kwamba hakuna filamu ni mapenzi tu.
IJUMAA LAFUKUNYUA, LAIBUKA NA PICHA
Kama kawaida ya Magazeti ya Global Publishers, liwe Ijumaa, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Amani, Championi au Risasi ni kuchimba mambo kwa undani na kuupata ukweli wa jambo, hivyo timu ya wanahabari wetu ilizama mitaani na kuzisaka picha za filamu hiyo.
Julai 23, 2013, Ijumaa lilifanikiwa kuzipata picha hizo ambazo moja baada ya nyingine zinawaonesha Lucy na Ndikumana wakiwa katika mapozi mbalimbali ndani ya filamu (angalia picha)
.
MWANZO, MWISHO NI WAWILI TU!
Katika picha hizo ambazo ziko mikononi mwa dawati la Ijumaa, wasanii walioonekana ni Lucy na Ndikumana tu hivyo kushibisha yale maswali ya Uwoya kuwa ni kwa nini filamu nzima ichezwe na watu wawili tu?
HADITHI YA FILAMU YADAIWA NI KISA CHA KWELI CHA UWOYA NA NDIKU
Habari za hivi karibuni zilisema kuwa,   cha ajabu, kisa kinachosimuliwa katika filamu hiyo ni cha kweli.
Ilidaiwa kuwa kisa hicho kilimpata Ndiku baada ya kukutana na Uwoya kwa mara ya kwanza kabla ya kufunga ndoa.
Madai hayo yanaongeza chachu katika moyo wa Uwoya na kuzidi kuamini kuna kitu kinaendelea kati ya mumewe na Lucy.
UWOYA AKATISHA ZIARA SWAZILAND
Uwoya alipotafutwa na Ijumaa juzi ili kumsikia msimamo wake kuhusu hali tete katika ndoa yake baada ya hisia zake kuwa anaibiwa mumewe na Lucy, alisema atapasua jipu atakapotua Bongo akitokea nchini Swaziland ambako alikwenda kwa ziara binafsi.
Alisema kuwa amelazimika kukatisha ziara na kurudi Tanzania kwa vile suala la Lucy na mumewe linamnyima raha kuendelea kuwepo ugenini.
“Narudi Bongo Jumatano (juzi). Unajua hili suala limeninyima raha kabisa. Siwezi kuendelea kuwepo huku ugenini. Nikifika nitatoa la moyoni,” alisema Uwoya.
LUCY AZUNGUMZA KUTOKEA DENMARK
Wakati Uwoya akizungumza kutokea jijini Mbabane, Swaziland, Lucy yeye alitoa sauti yake akiwa nchini Denmark kwenye Jiji la Copenhagen.
Alipoulizwa kuhusu tambo za Uwoya baada ya yeye kucheza filamu na mumewe Ndikumana, alijibu:
“Mimi sina cha kusema, yeye anajua mimi ni nani katika filamu. Mumewe kaonesha mapenzi ye kucheza filamu yangu, sasa anaposema ningemtaarifu yeye kama nacheza filamu na mumewe ili iweje? Kwa nini asimlaumu mume wake ambaye ndiye alipaswa kumtaarifu?” alisema Lucy.
Lucy aliongeza: Kama Ndiku angekuwa mtoto chini ya miaka kumi na nane nataka kucheza naye filamu hapo kweli, ningepaswa kumtaarifu Uwoya kama mama mtu, lakini mume, si sahihi kunilaumu.
MADAI YA HADITHI YA FILAMU KUWA KISA CHA KWELI
Kuhusu madai kwamba hadithi ya kwenye filamu hiyo ni kisa cha kweli kati ya Uwoya na Ndiku, Lucy alijibu:
“Teh! Teh! Si kweli bwana. Kama Uwoya ndiyo kasema hivyo basi ana kisa kinachofanana na cha filamu yangu. Mimi filamu ni yangu na hadithi ni yangu.”
WAONGOZA FILAMU BONGO WANASEMAJE KUHUSU WATU WAWILI TU?
Ili kujifunza juu ya wasanii wawili kucheza filamu nzima, Ijumaa liliwatafuta baadhi ya waongoza filamu Bongo.
Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’: Kusema kweli ni vigumu sana. Labda kama zile filamu za porini, mtu anakimbizwa na wanyama (documentary).
“Lakini kucheza filamu za mjini halafu wawili tu, mnagombana wenyewe mnapatana wenyewe ni kazi sana,” alisema Chuz.
Jacob Steven ‘JB’: Du! Labda kama utakuwa umekusudia kupunguza bajeti, lakini pia haitakuwa filamu nzuri, wawili tu?! Kwanza ni filamu gani hiyo ya watu wawili tu?
Ijumaa lilimkatia simu.
Mahsin Awadh ‘Dk Cheni’: Mh! Zipo kama mtu mwenyewe atakuwa ameamua, lakini sidhani kama sokoni itakubalika. Ni nani huyo kwani?
Ijumaa likamkatia simu.
Wazoefu wengi wa filamu walisema documentary ndizo zinaweza kuwa na watu wawili lakini si filamu.

source-GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Emmanuel Mgana27 July 2013 at 07:30

    Jamani Watanzania wenzangu, chonde chonde kuweni na utu moyoni, hata kama alikukosea huu sio ubinadamu bali ni unyama usio na huruma. Tuna muombea apone haraka, na atakae bainika achukuliwe hatua za kisheria.

    ReplyDelete
  2. Wewe mbna umechoma bhana!

    Ni nan unayemuombea apone coz naona km umepiga mbz nch kavu o ?

    ReplyDelete
  3. ata wewe ulimsaliti

    ReplyDelete
  4. Hiyo ni vipande vya filamu

    ReplyDelete
  5. Hiyo ni vipande vya filamu

    ReplyDelete
  6. yuko sawa kwan hata wewe huwa unafanya huo uchafu

    ReplyDelete

Top Post Ad