HUYU NDIYE MTANZANIA ALIYEUWAWA NA VIBAKA JUZI ALHAMISI NCHINI MAREKANI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku.

Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili.


Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya jirani.

“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote”
alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC
alipohojiwa na News4.

Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa.

“Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4.

Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana.
Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.

Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:

“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wa
nafunzi wote watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad