MAISHA YA OSAMA KABLA HAJAKAMATWA YAFICHULIWA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TUME ya Abbottabad imesema kuwa Osama bin Laden aliishi kama mtu wa kawaida bila wasiwasi wowote kwa karibu miaka 10 na aliwahi hata kusimamishwa na polisi katika eneo la Swat huko Pakistan kwa kupeleka gari kwa kasi mno, lakini hakukamatwa.
Ripoti hiyo iliyofichuliwa na Televisheni ya al Jazeera na kuoneshwa juzi jioni, inaonesha kinagaubaga maelezo ya kusisimua kuhusu maisha ya Osama bin Laden, mtu hatari aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba, na aliyekuwa akivaa kofia la mchunga ng’ombe katika tambarare za Marekani, kuepuka kugunduliwa kutoka angani.
Ripoti hiyo ya kurasa 336, iliandikwa na tume ya Abbottabad inayoongozwa na jaji na iliyoundwa na Serikali ya Pakistan muda mfupi baada ya vikosi maalumu vya Marekani kumuua bin Laden Mei 2 mwaka 2011. Misingi ya ripoti hiyo ni mahojiano yaliyofanywa na vyanzo 201, wakiwemo jamaa wa familia yake na maofisa mbalimbali.
Matokeo ya uchunguzi huo ambayo hayajachapishwa rasmi, yanajumuisha ushahidi wa uzembe mkubwa katika karibu kila ngazi ya vyombo vya usalama vya Pakistan.
Ripoti inakosoa vikali namna Marekani ilivyofanya uvamizi katika makazi ya bin Laden huko Abbottabad, ikisema ilichukua hatua kama jambazi mhalifu. Inauweka katika kiti moto utawala wa Pakistan kwa kushindwa kugundua shughuli za Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), katika ardhi yake, na hautupilii mbali uwezekano wa kuhusika maofisa walaghai katika idara ya ujasusi ya Pakistan, suala tete kuligusia katika uchunguzi wa hali ya juu namna hiyo.
Ripoti inatoa maelezo kuhusu usiku wa kifo cha bin Laden na kutoa taswira ya mtu aliyekuwa akibabakia na kama mwenda wazimu ambaye kila mara alikuwa mbioni kukwepa kutiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Bin Laden aliwasili nchini Pakistan msimu wa machipuko mnamo mwaka 2002, na wakati mmoja aliishi Haripur kwa miaka miwili kabla kuhamia katika makazi yake ya mjini Abbottabad na familia yake kubwa mnamo Agosti 2005.
Ripoti inasema maeneo yote alikoishi hayajulikani kikamilifu, lakini miongoni mwao ni FATA yani Waziristan kusini na Bajaur, Peshwar, Swat na Haripur.
Ripoti imegundua bin Laden aliingia Pakistan akitoa eneo la Tora Bora nchini Afghanistan, ambako majeshi ya Marekani yalikuwa yakimsaka mwaka 2002. Familia yake ilihamia Karachi, Pakistan kutoka Kandahar, muda mfupi baada ya mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani dhidi ya jengo la Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO) mjini New York, makao makuu ya wizara ya ulinzi, Pentagon nje ya mji wa Washington, na uwanja mmoja huko Pennsylvania.
Osama hakupenda mali
Katika ushuhuda wao wake wa bin Laden walisema hakupenda sana mali zake binafsi na alikuwa na nguo chache sana. Ripoti hiyo imesema kabla kwenda Abbottabad bin Laden alikuwa na mavazi matatu ya kitamaduni yajulikanayo kama shalwar kameez aliyoyavaa wakati wa msimu wa kiangazi na mengine matatu kwa ajili ya msimu wa baridi.
Wakati alipojihisi anaugua, Osama bin Laden alijitibu mwenyewe kutumia dawa za kienyeji za Kiarabu. Kwa mujibu wa ripoti zisizo rasmi za Marekani, bin Laden alikuwa akiugua ugonjwa wa Addison, upungufu wa adrenalini mwilini, na kila mara alipojihisi mvivu angekula tufaha na chokoleti.
Maofisa wa Serikali na usalama nchini Pakistan hawakuweza kupatikana ili kutoa kauli kuhusu ripoti hiyo. Baadhi ya maofisa wa Marekani wameelezea wasiwasi wao wakiyashuku mashirika ya ujasusi ya Pakistan kwa kumlinda bin Laden, lakini Pakistan imelipuuzilia mbali wazo hilo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu jamaa kama kufa amefariki 2 mwenyewe..ingekuwa ni kweli hawa marekan walimkmata wangemtembeza dunia nzima

    ReplyDelete
  2. Innocent safari11 July 2013 at 10:19

    Siamin kweli kama marekan ilimuua osama kwan hakuna ushahid wowote ulioonekana.hata hivyo vitendo wanavyofanya amerika vya mauji kuanzia sadam,osama na wengine na kufunga watu wengine wasiokua na hatia huko gerza la gwantanamo nchin cuba ni dhambi kubwa na ipo siku watasimama kujibu mbele ya haki

    ReplyDelete
  3. inawezekana ni yy walie mkamata,maana asingekaa kimya hivyo,jamaa wako fit sana hawana 7bb zakudanganya.

    ReplyDelete
  4. Inatakiwa iwepo siku ya Osama Duniani, maana ili tuwe tunakumbuka alikufa lini.

    ReplyDelete

Top Post Ad