MAKAMBA: JE DSTV IMEWASHINDA KUHUSU CHANNEL 5 ZA BURE?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majuzi tulisikia mgogoro kati ya kituo cha Television cha Star na Kampuni ya Startime na tishio la Startv kujitoa. Wizara na Tume ya mawasiliano wakaingilia kati na kuwalazimisha Startv wapitishe matangazo yao Startimes ili kukidhi kigezo cha kampuni zenye ving'amuzi kurusha matangazo ya Bure ya vituo vitano kitaifa ambvyo ni TBC1, ITV,STAR TV,CHANNEL 10 na CHANNEL 5.

Ajabu ni kuwa mbona jambo hilo limeshindikana kwa DSTV? Mwenye kutumia kutumia kingamuzi cha kampuni ya Multichoice (DSTV) ni lazima uwe na kingamuzi kingine maana kama fedha imekata DSTV HUWEZI pata matangazo ya hizo channel za bure bila malipo.

Je, wizara yako na tume ya mawasiliano mumewashindwa hao wawekezaji? Maana kama suala hilo kwao halipo mbona channel za kichina zinaonyeshwa bure?

Hii inamaanisha serikali yetu ina katabia ka kuwaogopa wawekezaji bila kujali maslahi ya wananchi wao?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Fanya utafiti kabla ya kupost usije ukapost pumba. Dstv na Zuku wamesajiliwa na TCRA kama Pay tv. Hawana kibali cha kurusha local channels bure cos hata wao wananunua. Zuku wanadai wanafuatilia kupata leseni lakini hawafungwi na sheria.

    ReplyDelete

Top Post Ad