MASKINI:MWANAFUNZI AJILIPUA NA MAFUTA YA PETROL

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mamae..huyo ni kumtandika viboko hata kama amekufa

    ReplyDelete
  2. kujiua kwa sisi vijana wengi nw days inatokana na sababu nyingi ila chache ni vijana wengi kutojua wanachokitaka kwenye maisha yao simply lack of focus na kutokumcha mungu plus kukosa shule kichwani..

    ReplyDelete
  3. Kukimbilia mambo yasiyomuhusu. Uliona wap elimu na mapenzi. Asijali uko kuzim atalipuliwa sana na iyo Petro liya.

    ReplyDelete

Top Post Ad